LAYIII
Yemi Alade ni msanii maarufu kutoka Nigeria ambaye alitamba sana na ngoma yake Johnny. Nimekutana na interview moja aliofanya msanii huyu jijini Lagos, aliulizwa maswali mengi lakini moja kubwa lilikuwa linahusu hali ya wasanii kupeana support kwenye muziki.
Yemi Alade alikuwa na haya ya kusema.
>>> “siwezi
kuzungumza kwa niaba ya kila mtu so nitaongea kulingana na mtazamo
wangu, kwa mimi binafsi nahisi kwenye industry wanaume wanapeana support
zaidi kuliko wanawake, sijui kwa nini ila naona hii ndio hali halisi
kwa hapa kwetu.”
>>> “wanaume
wanapeana support kirahisi sana… kwa mfano mwanaume kumshirikisha
mwanaume mwenzake ni rahisi sana, wanaweza tu wakawa wanapiga stori
alafu stori za studio zikazuka mmoja akamuelezea mwenzake shida yake na
vitu kama hivyo, basi kupitia kusadiana unakuta wameshirikiana kwenye
wimbo”.
>>> “wanawake
sasa, kwanza tunazinguana mno na kupeana wakati mgumu… mara utasikia
niko studio mummy nitakucheki nikitoka, na hata wakishirikiana wataleta
ushindani flani, watafika kwenye show mida tofauti, yote makusudi tuu,
kutafuta attention na tunasahau kazi ni yetu sote. Wanaume hawako hivi”. <<< Yemi Alade.
No comments:
Post a Comment