LAYIIII
Kama uliwahi kuweka vocha kwenye simu
yako alafu ukakuta ile hela uliyoweka haipo na wala hujaitumia, hii ishu
imewagusa Wabunge… Alianza Mbunge kwa kuuliza swali kwamba nini
kinafanyika kuzuia wizi wa aina hiyo.
“Kumekuwa
na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanapoteza pesa kujiunga na
vifurushi ama wanaponunua vocha… Serikali itachukua hatua gani kudhibiti
Makampuni ya simu ambayo yanafanya wizi kwa wananchi” >>> Mbunge Murtaza Mangungu.
“Kumekuwa
na udhaifu mkubwa kwa upande wa TCRA kwenye kufuatilia malalamiko ya
watu pale ambapo wanadhurumiwa, watu wanatoa malalamiko kwa Makampuni ya
simu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa” >> January Makamba.
“Serikali
imetoa onyo kwa TCRA kwamba tunataka hatua zianze kuchukuliwa na namna
mpya ikiwemo kuhakikisha kwamba kuna kituo ambacho kipo saa zote kwa
ajili ya kupokea simu na malalamiko ya watu na ni rahisi kituo hicho
kufikika na watu wanahakikishiwa majibu, malalamiko yasiposhughulikiwa
ndani ya saa 48 hatua za Kisheria zinachukuliwa kwa makampuni ya simu” >>> Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
No comments:
Post a Comment