Monday 29 June 2015

Msanii wa Afrika aliyegoma kwenda kwenye tuzo za BET kwa makusudi, dharau imehusika..

LAYIII
Fuse ODG 2Kitendo cha BET ambayo ni Television kubwa ya Marekani kwenye ulimwengu wa burudani kuwapa Wasanii wa Afrika tuzo zao kwa time tofauti na tuzo wanazoshinda wasanii wakubwa wa Marekani kama Beyonce na Chris Brown kiliwahi kulalamikiwa na wengi akiwemo Ommy Dimpoz.
Hata Davido aliposhinda mwaka jana kwenye sehemu ya Interview Diamond alieleza kwamba tuzo za wasanii wa Afrika huwa hazitolewi pamoja na zile za kina Beyonce, wasanii kwenye kipengele cha Afrika waliitwa asubuhi na mapema wakati ukumbi ukiwa mtupu bila watu ndio mshindi akakabidhiwa tuzo alafu badae jioni ndio kina Beyonce wakakabidhiwa kwenye event yenyewe lakini ukitazama kwenye TV huwezi kugundua sababu wanaunganisha kijanja.

fuse 20Baada ya hayo yote, mwimbaji staa Mwafrika ambaye makazi yake ni Uingereza FUSE ODG ametangaza wazi kwamba sababu za yeye kutokwenda kwenye tuzo hizo mwaka huu ni kwa sababu tuzo hizo hazitolewi sawa na za kina Beyonce.
Fuse ambaye alikua anawania tuzo kwenye tuzo hizi za BET mwaka huu amesema mambo ya kupeana tuzo backstage inaonyesha kabisa BET hawawaheshimu wasanii wa Afrika wanavyojituma kwenye kazi zao.


Fuse ODG





No comments:

Post a Comment

advertise here