LAYIII ON SPOT
Dwayne Johnson maarufu kama The Rock ni mwigizaji, movie producer na mchezaji mieleka kutoka Marekani aliejitengenezea jina kubwa kwenye mieleka na kufanya apate shavu kubwa kwenye movie za action Hollywood, Marekani.
The Rock ameweka wazi sababu za yeye kuacha mchezo wa mieleka…
Dwayne Johnson maarufu kama The Rock ni mwigizaji, movie producer na mchezaji mieleka kutoka Marekani aliejitengenezea jina kubwa kwenye mieleka na kufanya apate shavu kubwa kwenye movie za action Hollywood, Marekani.
The Rock alichukuwa time na kufanya interview na gazeti la Marekani Esquire na kuongelea mambo mengi ikiwemo sababu zilizomfanya aingie kwenye tasnia ya uwigizaji pamoja na mafanikio yake binafsi. The Rock alikuwa na haya ya kusema:
Kuhama kwenye mieleka kwenda kwenye uwigizaji:“Baada
ya kufanikiwa kwenye mieleka, nilihamasika kujabiru uwigizaji wa movie
za action, na nimefika hapa nilipo kwa kutumia nidhamu niliojinfunza
kwenye mieleka, kujenga ukaribu na watu kwenye industry, na kujiunga na
madarasa ya kuigiza”.
Kama anapendelea uwigizaji zaidi kuliko mieleka:“Mieleka ni
mpenzi wangu wa kwanza, lakini kwenye uwigizaji kuna upendo tofauti
ambao unaniruhusu mimi kugusa watu kupitia sanaa nyingine na pia
kutengeneza hela ndefu zaidi, movie zinanifundisha mambo mengi sana
ambayo nisingeweza kuyajua mwanzoni”.
Kama alichukuliwa serious alivyoanza kuigiza: “Haikuwa
rahisi hapo mwanzoni, kama Anorld Schwarzenegger niliambiwa nina mwili
mkubwa kuwa mwigizaji wa movie za action na nilinyimwa nafasi nyingi
lakini sikukata tamaa, na leo niko hapa kwa sababu sikuchoka”.
No comments:
Post a Comment