Wednesday 1 July 2015

Liverpool yakamilisha usajili wa mchezaji wa sita leo hii.

LAYIII
Dirisha la usajili wa kipindi cha kiangazi limefunguliwa leo rasmi na klabu ya Liverpool imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine baada ya Firmino wiki iliyopita.
wiki iliyopita. 
 Liverpool wamemsaini Nathaniel Clyne kutoka Southampton kwa ada ya uhamisho ya £12.5m, na mchezaji huyo leo amesaini mkataba wa miaka 5.
“Nina furaha kutimiza ndoto yangu ya kuja hapa Anfield kuitumikia klabu kubwa kama hii,” Clyne aliuambia mtandao wa Liverpool.
“Mara tu baada ya Liverpool kuonyesha kunihitaji, Nilifurahia na nikapenda uhamisho huo ukamilike haraka.”
 
Clyne, ambaye alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Southampton, sasa anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool.

No comments:

Post a Comment

advertise here