Wednesday 1 July 2015

Watanzania waliopewa tuzo na malkia wa Uingereza ndio hawa wamerudi Tanzania

layii

.
.
Stori ninayotaka kukusogezea sasa hivi ni hii kuhusu vijana wawili kutokea Tanzania (Given Edward & Angel Benedicto) ambao wiki iliyopita walikabidhiwa tuzo na malkia wa Uingereza kutokana na
kile walichokifanya kwa jitihada zao.
Vijana walioteuliwa kuwania tuzo hizo za malkia wa Uingereza walikuwa 60 kati ya mamia ya washiriki na dhumuni kubwa ni kuwapongeza  kwa mchango wao mkubwa wa kimaendelea katika nchi zao.
.
.
Akizungumza na waandishi wa habari leo July 1, 2015 Given Edward ambaye alikabidhiwa tuzo na malkia wa Uingereza alisema..’Kuna rafiki yangu mmoja aliona shughuli ninazofanya akaniambia kuwa kuna tuzo zinatolewa na malkia na anaamini kuwa naweza kupata kutokana na kushughulia ninayoifanya’
Given 1‘Walihitaji interview ambazo niliwahi kufanya na waandishi mbalimbali wakazihitaji  kuhusu project zangu  na wakataka na makampuni  niliyowahi kufanya nayo kazi baada  ya hapo basi wakatutangaza’
.
Given Edward.
Sasa hivi itakuwa ni  rahisi zaidi ninapoenda kuongea  na mashiriki au makampuni  kwasababu ninalofanya linathaminiwa lakini pia hata kwa  vijana wenzangu sasa hivi  itakuwa rahisi kwangu kufanya nao kazi kutokana na kile ninachokifanya kwani nina mipango mikubwa  zaidi ya hapo lengo langu ni kafanya process nzima ya kusoma  iwe rahisi zaidi na wanafunzi  wawe wanapenda zaidi kusoma  kwasababu sasa hivi wanafunzi  wengi wanachukulia kusoma kama adhabu kuliko kama zawadi..’alisema
.
.
Wa pili ni Angel Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani (House Girl) alimaliza kidato cha nne akaona aweza kuendelea na masomo, hali ni ngumu kwenye kimaisha akawa ni mfanyakazi wa ndani au msichana wa kazi za ndani (House Girl) lakini leo hii ameweza kutumia nguvu yake ya ushawishi ya kuongea na vijana na kazi yake imetambuliwa na malkia na akapewa tuzo.
.
Angel Benedicto.
Akizungumza na waandishi wa habari leo July 1, 2015 Angel Benedicto alisema…’Tuzo hii inanisaidia kwamba niweze kuwafikia vijana zaidi ambao ni wafanyakazi wa nyumbani hasa wa kike ambao wamekata tamaa tuweze kuwasaidia kwamba haujazaliwa kuwa mfanyakazi wa nyumbani tu , kuna nafasi nyingi pia kwa hiyo kama ni ujasiriamali jitahidi  kama unapata elfu 40 yako tunza…

No comments:

Post a Comment

advertise here