LAYIII
Jana mji wa Bagamoyo uliingia katika taharuki kubwa baada ya habari kuenea kuwa kuna marehemu kafufuka baada ya kuthibitishwa na madaktari kuwa amefariki.
Jana mji wa Bagamoyo uliingia katika taharuki kubwa baada ya habari kuenea kuwa kuna marehemu kafufuka baada ya kuthibitishwa na madaktari kuwa amefariki.
Timu ya Hekaheka ilifunga safari hadi
Bagamoyo na kukuta umati wa watu katika nyumba ambayo marehemu alikua
akiishi ikiwa ni muda mchache baada ya mwili wake kurejea kutoka
hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo ndipo alipofariki.
Utata wa marehemu kufufuka Bagamoyo upo kwenye Hekaheka ya leo…(Audio)
Jana
mji wa Bagamoyo uliingia katika taharuki kubwa baada ya habari kuenea
kuwa kuna marehemu kafufuka baada ya kuthibitishwa na madaktari kuwa
amefariki.
Timu ya Hekaheka ilifunga safari hadi
Bagamoyo na kukuta umati wa watu katika nyumba ambayo marehemu alikua
akiishi ikiwa ni muda mchache baada ya mwili wake kurejea kutoka
hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo ndipo alipofariki.
Majirani walidai baada ya mwili wa
marehemu huyo kurudishwa nyumbani ili kuanza taratibu za mazishi
walishangaa kuona bado mwili wa moto na alikua akijitingisha wakati
waoshaji wakimuandaa kwa ajili ya kumzika.
Shangazi wa marehemu alisema ni kweli
baada ya kumleta walishangaa mwili ukiwa wa moto na mapigo ya moyo
yakifanya kazi kama kawaida licha ya madaktari kuthibitisha kuwa
amefariki, na wakaamu kusimamisha shughuli za mazishi hadi kesho yake
walipoona amekuwa wa baridi na tayari alishafariki.
Daktari aliyethibitisha kama marehemu
amefariki alisema baada ya kumpima marehemu alikua amefariki na kuruhusu
taratibu ziendelee, na alisema kuwa mwili wa marehemu kuwa wa moto
inategemee na mazingira ya sehemu alipohifadhiwa.
Isikilize stori kamili hapa mtu wangu…
No comments:
Post a Comment