Tuesday, 30 June 2015

Arsenal yampa Cech mkataba miaka minne

LAYIII
Hatimaye yametimia kwa Arsenal kupata saini ya mlinda mlango Petr Cech kutoka Chelsea kwa kitita cha pauni milioni kumi.
Mlinda mlango huyo wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Czech, ambaye amecheza zaidi ya mechi 400 katika misimu 11 akiwa na timu ya Chelsea, amejiunga na Arsenal the Gunners kwa mkataba wa miaka minne.
Cech, mwenye umri wa miaka 33, alicheza mechi saba tu msimu uliopita baada ya nafasi yake kunyakuliwa na mlinda mlango kutoka Ubelgiji Thibaut Courtois.
Cech amesema alifikiri angestaafia Stamford Bridge, alakini ameongeza kusema: "Maisha daima hayawi vile unavyofikiria yakawa."
Ameandika: "Msimu ulioopita wa kiangazi, mambo yalibadilika na nikaelewa kuwa sikuwa mlinda mlango chaguo la kwanza, lakini nilifikiria haukuwa wakati mzuri kwangu kuondoka.
"Wakati wa msimu huo, ilieleweka wazi kuwa hali yangu isingebadilika na kama ninavyofahamu siko katika kazi yangu ambapo nastahili kuwa- Niliamua kuondoka na kutafuta changamoto mpya."
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anasema: "Petr Cech ni mchezaji ambaye nimemtamani kwa muda mrefu na nimefurahi sana ameamua kujiunga nasi."
Cech, alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Rennes ya Ufaransa Julai 2004 na kushinda makombe 13 akiwa na Chelsea - likiwemo kombe moja la klabu bingwa na mataji manne ya ubingwa wa ligi kuu ya England.

No comments:

Post a Comment

advertise here