TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo,
anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu
Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central)
akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba,
mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye
orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo,