Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano.
JIFUNZE GRAPHICS KWA DAKIKA CHACHE TU KWA USUBSCRIBE KATIKA CHANNEL YETU YA SWAXBZ TV SHOW
“Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile taarifa kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya ilivuja, hadi wachungaji wenzangu walininyanyapaa, nikivaa suti au nikiendesha gari kila anajua ni pesa za madawa” alisema Mzee wa Upako
Mzee wa Upako ameshauri vita ya dawa za kulevya kwa watu wanaotuhumiwa ni bora viongozi wangetumia njia za kipolisi kuwataka kufika polisi kwani kutumia njia ya magazeti inaweza kushusha heshima ya baadhi ya watu ambayo wameijenga kwa miaka mingi.
“Mimi kutokana na tuhuma zangu kuvuja kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya niliishi miaka saba watu wananinyayapaa, tena hiyo ni tuhuma tu. Imenichukua miaka saba kusafisha jina, nimekuja kuanza kusafisha jina mwaka 2005 hivi”
Mchungaji huyo alisema hata yeye binafsi anachukia sana dawa za kulevya kutokana na madhara yake kwa jamii, hivyo hawezi kuthubutu kujihusisha nazo wala hawezi kuunga mkono watu wanaofanya shughuli hizo kwa kuwa dawa za kulevya zinaua kizazi cha maendeleo na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment