Thursday 9 February 2017

LECEISTER CITY YAZIDI KULINDA HESHIMA YAKE



Leiceister city na Derby County wakichuana

Klabu ya soka ya Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima katika uwanja wake wa nyumbani wa king power kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Derdy County katika michuano ya mwaka huu ya FA CUP ukiwa ni mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya michuano hiyo.

Hadi dakika 90 za mchezo zina maliziaka timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-
1 na kulazimia kuongezwa kuda wa ziada.

Leiceister city ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Andy King ,na baadaye Derdy County wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Abdoul Camara, huku Onyinye Wilfredy Ndindi akiongeza bao la pili kwa upande wa Leceister city katika dakika ya 94 muda wa nyongeza.

Dakika ya 114 Demaria Gray akapigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Derby County kwa kuandika bao la tatu na la mwisho.

Kwa matokeo hayo sasa Leiceister city watakutana na Milwall katika raundi ya tano wakiwa ugenini.

No comments:

Post a Comment

advertise here