Thursday 9 February 2017

ZIGO LAMPAGAWISHA BOB JUNIOR KINOUMA NOMA

Stori: Na Andrew Carlos IJUMAA | ShowBiz
Ama kweli kuna watu wamejaaliwa! Msanii wa muziki Bongo, Bob Junior hivi karibuni alijikuta akishindwa kurekodi video ya wimbo wake wa Chukuchuku baada ya kuchanganywa na dada mmoja aliyemtumia
kama modo ambaye kafungashia ile mbaya.


‘Zigo’ lilivyompagawisha Bob Junior.
Ilikuwa kwenye jengo moja lililopo Posta jijini Dar ambapo  Bob Junior akiwa na wenzake walifika eneo hilo kwa ajili ya kurekodi lakini ilipofika ile ‘scene’ ya modo huyo kumkatia viuno, msanii huyo akajikuta amekodoa macho kodo na kushindwa kufanya alichokuwa akitakiwa kufanya.

Shughuli ya kuandaa video ilivyokuwa ‘taiti’ kwa upande wa Bob Junior
“Unaambiwa yule demu kafungashia ile mbaya, sijui kamtoa wapi! Yaani kuna wakati Bob Junior badala ya kucheza kama ilivyopangwa, alijikuta akikodolea macho zigo la dada huyo,” alisema mmoja wa marafiki wa msanii huyo aliyekuwa eneo la tukio.

Director akimuelekeza jambo Bob Junior



Kazi ikiendelea

No comments:

Post a Comment

advertise here