Friday, 10 February 2017

MENGINE YAIBUKA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kujiridhisha na kiwango cha mapato linayokusanya kwa usafirishaji mizigo iwapo kiko sahihi.

Majaliwa amesema hayo alipotembelea makao makuu ya ATCL jijini Dar es Salaam kujionea utendaji tangu lilipoboreshwa mwaka jana kwa kununuliwa na Serikali ndege mpya mbili.

Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga kuhakikisha anatekeleza suala hilo.


Pia, ametakaka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba za njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.

Vievile amesema ataagiza uchunguzi ufanywe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) utakaolenga kujua ukusanyaji mapato katika kipindi hicho.

Waziri Mkuu akasema Serikali haitakuwa tayari kushuhudia shirika hilo linakufa tena na kuwataka viongozi wahakikishe linaendeshwa kwa faida kwa manufaa ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

advertise here