Friday 10 February 2017

VURUGU ZATAWALA BUNGENI WABUNGE WAKIMPINGA RAIS..MABOMU YARINDIMA


Bunge la Afrika kusini jana lilijawa na vurugu kuipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.

Wakati akianza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa.

Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa,
ulifanywa pia na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala.

Awali nje ya bunge la nchi hiyo, Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu, ili kuweza kuwasambaratisha.

Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa hotuba yake.
Via>>BBC
KUTANA NA BARABARA AMBAZO NI ZA HATARI ZAIDI DUNIANI

No comments:

Post a Comment

advertise here