Klabu ya AC Milan imeripotiwa kuwa katika harakati za kutaka kuwasajili washambuliaji wanaocheza katika ligi ya nchini England Romelu Lukaku wa Everton pamoja na Alexis Sanchez wa Arsenal.
Wawili hao wanatajwa kuwa kwenye mipango ya klabu hiyo ya mjini Milan, itakapofika mwishoni mwa msimu huu, na tayari imearifiwa fungu la pesa limetengwa kwa ajili ya uhamisho wao.
Gazeti la Daily Express, limefichua siri hiyo baada ya kufanywa kwa uchunguzi wa kina na kubainika kuwa, viongozi wa AC Milan wanaamini endapo watawasajili washambuliaji hao, watafanikisha azma ya kurejea katika kilele cha mafaniklio kama ilivyokua miaka ya nyuma.
Gazeti hilo limedai kuwa, kiasi cha Pauni milioni 45 kimetengwa kwa ajili ya mshambuliaji Sanchez, mwenye umri wa miaka 28, huku mshahara wake ukitarajiwa kuwa Pauni 250,000 kwa juma ambao ameitaka klabu ya Arsenal kumlipa katika mkataba wake mpya.
Kwa upande wa Lukaku kiasi cha Pauni milioni 40 kinadaiwa kutengwa kwa ajili yake, huku ikisemekana huenda mshambuliaji huyo kutoka nchini Ubelgiji akapokea mshahara wa Pauni 200,000 kwa juma.
No comments:
Post a Comment