Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano.