Saturday, 11 February 2017
KAMISHNA MPYA DAWA ZA KULEVYA AFUNGUKA


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Rogers Sianga kuwa kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).
Baada ya kuteuliwa Sianga alizungumza na Mwananchi na kusema kwanza anamshukuru Mungu kwa uteuzi huo na akaahidi kushughulikia kwa karibu kesi za vinara wa ‘unga’.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais jana, Gerson Msigwa ilisema Sianga atasaidiwa na Mihayo Msikela atakayekuwa Kamishna wa Operesheni na Fredrick Kibuta atakayekuwa Kamishna wa Intelijensia.
Uteuzi huo umekuja siku chache baada ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) kumtaka
SPIKA WA BUNGE AKEMEA TABIA YA WABUNGE KUKAMATWA KIBABE BUNGENI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amekemea tabia ya ukamatwaji wa wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na kusema kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu.
Akihitimisha mkutano wa sita wa Bunge, Ndugai amesema kama kuna kiongozi yeyote wa serikali anamuhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala ya kwenda
Friday, 10 February 2017
MENGINE YAIBUKA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kujiridhisha na kiwango cha mapato linayokusanya kwa usafirishaji mizigo iwapo kiko sahihi.
Majaliwa amesema hayo alipotembelea makao makuu ya ATCL jijini Dar es Salaam kujionea utendaji tangu lilipoboreshwa mwaka jana kwa kununuliwa na Serikali ndege mpya mbili.
Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga kuhakikisha anatekeleza suala hilo.
Pia, ametakaka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba za njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
Vievile amesema ataagiza uchunguzi ufanywe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) utakaolenga kujua ukusanyaji mapato katika kipindi hicho.
Waziri Mkuu akasema Serikali haitakuwa tayari kushuhudia shirika hilo linakufa tena na kuwataka viongozi wahakikishe linaendeshwa kwa faida kwa manufaa ya Taifa.
MAJIBU YA MAALIM SEIF BAADA YA PROF LIPUMBA KUMTAKA WAYAMALIZE
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Maalim Seif alitoa kauli hiyo kwenye ziara ya siku nne kwenye wilaya saba za mikoa mitatu ya Unguja.
Maalim alisema ataendelea kufuata taratibu za kisheria ili kuhakikisha chama kinamaliza moja kwa moja mgogoro aliodai umepandikizwa na CCM kupitia kwa Lipumba.
Thursday, 9 February 2017
ANITHA ATENGEWA DAU LA ILIONI KUMI ACHEZE UTUPU HUKO NOLLYWOOD

Kwa mujibu wa Jarida la Vanguard, Anitha anayependa kupiga picha akiwa ‘ameyabusti’ matiti yake, alikuwa akichati na jamaa kutoka Marekani, Kane na kumng’ang’aniza kucheza filamu hizo za utupu zitakazokuwa zikimuingizia
ZIGO LAMPAGAWISHA BOB JUNIOR KINOUMA NOMA
Stori: Na Andrew Carlos | IJUMAA | ShowBiz
Ama kweli kuna watu wamejaaliwa! Msanii wa muziki Bongo, Bob Junior hivi karibuni alijikuta akishindwa kurekodi video ya wimbo wake wa Chukuchuku baada ya kuchanganywa na dada mmoja aliyemtumia
ASKOFU GWAJIMA AMFYATUKIA MAKONDA SAKATA LA KUTAJWA DAWA ZA KULEVYA

Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi
Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.
Gwajima : nilichelewa kidogo nikaamua kupanda helkopta yangu mpaka uwanjani kabisa.
LECEISTER CITY YAZIDI KULINDA HESHIMA YAKE
Leiceister city na Derby County wakichuana
Klabu ya soka ya Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima katika uwanja wake wa nyumbani wa king power kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Derdy County katika michuano ya mwaka huu ya FA CUP ukiwa ni mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya michuano hiyo.
Hadi dakika 90 za mchezo zina maliziaka timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-
Klabu ya soka ya Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima katika uwanja wake wa nyumbani wa king power kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Derdy County katika michuano ya mwaka huu ya FA CUP ukiwa ni mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya michuano hiyo.
Hadi dakika 90 za mchezo zina maliziaka timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-
JINSI MANJI ALIVYO WASILI KITUO CHA POLISI KATI CHA DAR ES SALAAM
Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.
Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.
Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi
MZEE WA UPAKO NAYE ALIWAHI KUWA MHANGA WA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano.
Wednesday, 8 February 2017
USHAIDI DHIDI YA KESI YA SCOPIONI MAPYA YAIBUKA DAKTARI AIBUA USHAIDI MZITO
Shahidi wa nne katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete, ameieleza Mahakama kuwa mtu aliyehusika kumtoa macho Said Mrisho alikuwa ni mzoefu wa vitendo hivyo na siyo wa kawaida.
Shahidi huyo, Dk Christine Mataka (52) ambaye ni daktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alitoa maelezo hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala alipotoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Njwete (34) katika kesi iliyopata umaarufu wa ‘kesi ya Scorpion’ kutokana na maelezo kwamba aliyefanya uhalifu huo ni Scorpion.
KUTAJWA KWA MBOWE DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA BUNGE LIMENUKA
Hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapo kesho kuhojiwa, imewachefua baadhi ya wabunge.
Wabunge waliohojiwa mjini Dodoma jana, walisema kinachoendelea ni siasa badala ya uhalisia.
Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT – Wazalendo), Zitto Kabwe alisema kinachoendelea ni siasa za kuchafuana na kwamba Makonda ajiandae kubeba msalaba wake katika jambo hilo.
VIDEO MAJIBU YA YUSUPH MANJI BAADA YA KUHUSISHWA NA MADAWA YA KULEVYA
Mfanyabiashara Yusufu Manji amesema kuwa atakwenda Kituo cha Polisi
kesho kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivyotaka.

Manji amesema kuwa pamoja na kuwa Makonda ametaka wafike Ijumaa yeye atakwenda kesho huku akihoji kuwa inawezekanaje wakaitwa watu 65 kuhojiwa kama hakuna shughuli za kufanya kwa siku nzima.
“Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa. Huwezi kunitangaza kupitia radio
Manji amesema kuwa pamoja na kuwa Makonda ametaka wafike Ijumaa yeye atakwenda kesho huku akihoji kuwa inawezekanaje wakaitwa watu 65 kuhojiwa kama hakuna shughuli za kufanya kwa siku nzima.
“Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa. Huwezi kunitangaza kupitia radio
VIDEO: ASKOFU GWAJIMA AJIBU MAPIGO KWA PAUL MAKONDA
Saa chache baada ya kutakiwa kufika polisi na mkuu wa mkoa kwa kutoa
taarifa juu ya madawa ya kulevya,Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima,Josephat Gwajima Amepost Ujumbe picha huu ambao wataalamu wa mambo
wanadai kuwa ni kama jibu kwa Mhe Makonda.
Subscribe to:
Posts (Atom)