LAYIII
Latiffah aka Tiffah hajamaliza hata siku moja lakini tayari ni staa si tu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari bali hata kwenye midomo ya watu wanaofuatilia burudani barani Afrika.
Wazazi wake mwenyewe wanamuita ‘The Next Most Famous Daughter in Africa.’ Kwa ukubwa wa Diamond Platnumz na mama yake Zari Ttale, hakuna ubishi kuwa Tiffah ana kila sifa ya kuja kuwa ‘binti maarufu zaidi barani Afrika.
Ikiwa ni saa chache tu tangu kuzaliwa kwake, akaunti yake ya Instagram iliyofunguliwa imefikisha followers zaidi ya 16,000.
Picha yake ya kwanza kuwekwa kwenye akaunti hiyo ina zaidi ya comments 860.