Sunday, 9 August 2015

HUYU NDO MWAFRIKA PEKEE ALIYE WAHI KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MIGUU DUNIANI

LAYIII
Ni kawaida kwa binadamu kufanya au kujifunza kitu zaidi ya kimoja lakini huwa ni watu wachache sana wanaoweza kuvimudu vyote kwa ufasaha, kwa rekodi tu wachezaji wote wanaotajwa kuwa bora duniani hawajawahi kuwa makocha wazuri licha ya kuweza kucheza mpira kwa ufasaha mfano kama Diego Maradona na hata Lionel Messi anatajwa hatokuja kuwa kocha mzuri kama akitaka kuja kuwa kocha.
George_Weah
Na wengine kama Pele na Zidane wao wameamua kabisa kutokuwa makocha, tukirudi Afrika hapa nakusogezea historia ya mwanasoka pekee kutoka Afrika aliewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia (Ballon d’or) 1995 George Ousman Weah kutokea Liberia huyu jamaa amemud
u kufanya vitu viwili kwa ufasaha aliamua kuwa mwanasiasa baada ya kuachana na soka.
1.1939597
George Ousman Weah ambae kwa sasa ni Senator wa Montserrado County anatajwa kuwa huenda atagombea Urais wa Liberia mwaka 2017 kupitia chama chake cha Congress for Democratic Change, kinachovutia na kushangaza wengi George Weah anaonekana kufanikiwa kwa awamu ya pili baada ile ya kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia wengi wanampa nafasi Weah kuingia ikulu ya Liberia mwaka 2017 kama ataamua kugombea.
MILAN, ITALY - JANUARY 06:  ITALIENISCHE LIGA 98/99; George WEAH/AC MAILAND - EINZELAKTION -  (Photo by Alexander Hassenstein/Bongarts/Getty Images)
Senator huyo wa Liberia aliwahi kutamba katika vilabu kadhaa barani Ulaya kama Monaco chini ya kocha wa sasa wa Arsenal Arsene Wenger 1988, PSG 1992 na klabu ya AC Milan ya Italia mwaka 1995 lakini mwaka 2004 FIFA ilimtangaza kuwa miongoni mwa wachezaji bora 100 wa Dunia waliohai.

No comments:

Post a Comment

advertise here