LAYIII
Baada ya kutoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Swansea City katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza, kocha wa Chelsea Jose Mourinho baada ya matokeo hayo hakupeleka lawama zake kwa muamuzi Michael Oliver ambae alimuonyesha kadi nyekundu golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois na kutoa penati kwa Swansea.
Mourinho lawama zake zote anapeleka kwa madaktari wa timu wakiongozwa na Eva Carneiro ambao waliingia uwanjani kumpatia matibabu Eden Hazard wakati wa dakika za lala salama
na kwa sababu mchezaji alipatiwa matibabu ni lazima atoke nje ya uwanja kitu kilichopelekea Chelsea kubaki na wachezaji 9 uwanjani.
“Sikufurahishwa
na daktari wa timu kwa sababu anatakiwa aelewe mechi ilivyo, hata kama
mtunza vifaa, doctor au Secretary ukiwa katika benchi unatakiwa uelewe
mchezo na unatakiwa kujua tuna mchezaji mmoja pungufu na unapoingia
uwanjani kumpatia huduma mchezaji unatakiwa kuhakikisha kuwa mchezaji
ana tatizo kubwa na nina uhakika Eden hakuwa na tatizo
kubwa”>>>Mourinho
No comments:
Post a Comment