LAYIII
TETESI~Juma Duni Haji kuwa Mgombea Mwenza wa Lowassa
Taarifa za gazeti la Uhuru la leo ni kuwa Profesa Lipumba kajiuzulu
uenyekiti CUF baada ya shinikizo kali kutoka kwa wanachama na viongozi
wa CUF wasiotoa rushwa wala kupokea rushwa wa upande wa Zanzibar
kutokana na sekeseke la yeye na al-maruhuni wenzie kumbeba Lowasa na
kutaka awe mgombea UKAWA.
Kwa kujiuzulu kwake kunaonyesha wazi kuwa Lowasa kupitishwa na UKAWA
itakuwa kazi ngumu kama CUF watatia ngumu UWEZEKANO AMBAO KWA SASA NI
MKUBWA MNO.
Kama atakatwa basi safari yake ya Matumaini hewa sijui itaelekea wapi.
Lakini taarifa zilizopo ni kuwa atatimkia ACT wazalendo kwa zitto kabwe
kujaribu karata yake ya mwisho.
TETESI~Juma Duni Haji kuwa Mgombea Mwenza wa Lowassa
Mtakumbuka kuwa hapo awali kulikuwa na minong'ono kwamba Dr Slaa ndiye
angekuwa Mgombea Urais wa UKAWA na mgombea mwenza wake angekuwa Juma
Duni Haji. Hata hivyo, kutokana na Lowasa kuteuliwa kuwa mgombea Urais
wa CHADEMA na ni dhahiri atakuwa mgombea wa UKAWA, Lowasa alimpendekeza
Ismail Jussa Ladhu kuwa mgombea mwenza wake. Hata hivyo, taarifa
zilizoripotiwa jana ni kwamba, Jusa alikataa pendekezo la kuwa Mgombea
Mwenza na hivyo viongozi wa UKAWA wakampendekeza aliyekuwa Mwanasheria
wa Zanzibar, Othman Masoud kuchukua nafasi hiyo.
Hata hivyo, taarifa mpya ni kwamba Othman Masoud naye amekataa pendekezo
hilo kwa madai kuwa ana mambo mengi ya kitaifa na kimataifa
yanamkabili. Kutokana na pendekezo hilo kugonga mwamba, ilibidi mpunga
utembee. Jana muda wa mchana, Maalim Seif Sharif Hamad akitumia usafiri
wa Makamu wa Kwanza wa Rais alienda Ofisi ya Lowasa iliyopo Masaki Dar
es Salaam akiambatana na mwanasiasa mkongwe, Juma Duni Haji. Kwenye
ofisi ya Lowasa alikuwepo Apson Mwang'onda, James Mbatia na Edward
Lowasa.
Viongozi hao kwa pamoja walitumia muda mwingi kumshawishi Juma Duni Haji
ili awe mgombea mwenza kama ilivyopangwa hapo awali. Hata hivyo, Juma
Duni alionekana kukataa hasa pendekezo la kumtaka ahame CUF na kujiunga
CHADEMA. Hata hivyo, viongozi hao walimhakikishia kuwa hakuna
atakachopoteza na kwamba kwa vyovyote itakavyokuwa, uanachama wake wa
CUF utalindwa. Lowasa alisema kuwa hawana muda zaidi wa kumtafuta
mgombea mwenza na kwamba tumaini pekee limebaki kwake Juma Duni Haji.
Baada ya kutafakari kwa muda kidogo, Juma Duni Haji alikubali pendekezo
hilo kwa masharti. Kwamba, apewe shilingi milioni 500 kama malipo yake
kwa kukubali kujivua uanachama wa CUF. Pia endapo UKAWA hawatashinda
nafasi ya Urais, awe analipwa mshahara wa shilingi milioni kumi kwa
mwezi kwa kipindi cha miaka 5 ambacho atakuwa nje ya siasa za Zanzibar.
Masharti hayo yamekubaliwa na Lowasa ambapo jana Juma Duni Haji amepewa
shilingi milioni 50 kama bonus na leo atapewa shilingi milioni 500
alizoomba na hivyo kufanya jumla ya kiasi chote atakachopewa kuwa
shilingi milioni 550.
Kutokana na hali hiyo, Juma Duni Haji anatarajiwa kutangazwa rasmi leo
Mlimani City Jijini Dar es Salaam ambapo CHADEMA wanafanya mkutano wa
kumtangaza mgombea Urais na Mgombea Mwenza.
Kwa haya yanayoendelea, yanatukumbusha kitu kimoja cha msingi. Kwamba,
CHADEMA hawakujiandaa kwa ajili ya kusimamisha Mgombea Urais na Mgombea
Mwenza. Mgombea Urais katoka CCM na Mgombea Mwenza wamemwazima kutoka
CUF. Hii inanikumbusha ya Mrisho Ngasa kuchezea Simba na Juma Kaseja
kusajiliwa na Yanga.
No comments:
Post a Comment