Tuesday 4 August 2015

BEKI HUYU MBIONI KUINGIA MAN U ..NI BAADA YA KUPOTEZA MATUMAINI YA KUMPATA RAMOS

LAYIII
Klabu ya Manchester United imekuwa ikimuwania beki wa Real Madrid ya Hispania Sergio Ramos kwa muda mrefu licha ya kuwa Real Madrid walikataa kumuuza beki huyo kwenda Manchester United kwani bado walikuwa wanahitaji  huduma yake. Man United walikuwa na matumaini ya kumsajili Ramos baada ya yeye kukiri kutokuwa na furaha Real Madrid.
1418670996_extras_noticia_foton_7_0
Baada ya Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez kutangaza kuwa wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba na Ramos, Man United wamebadili mawazo yao na kukubali yaishe
ila wamegeuzia mawazo na akili zao kwa beki wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid.
pepe-8
Man United wamegeuzia mawazo yao kwa Képler Laveran Lima Ferreira Pepe ambae amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Santiago Bernabeu, Man United bado wanaonyesha dhamira ya kweli ya kutafuta beki mwenye kiwango cha juu licha ya kuwa bado Madrid wanamuhitaji aongeze mkataba.
Real Madrid's Pepe from Portugal gestures during a Spanish La Liga soccer match against Levante at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, Spain, Sunday, Feb. 12, 2012. (AP Photo/Andres Kudacki)
Hata hivyo Man United bado wamesimamia msimamo wao wakutaka Pepe ahusishwe kwenye uhamisho wa golikipa wa Man United David De Gea kwenda Real Madrid kama ilivyokuwa kwa Ramos. Madrid wanafahamika kwa utamaduni wao wakutopenda
kumuachia mchezaji wanayempenda kirahisi kwani Pepe yupo na klabu hiyo toka mwaka 2007 akitokea FC Porto ya Ureno.


No comments:

Post a Comment

advertise here