LAYIII
Mmlaka ya chakula na Dawa TFDA
imeatoa ripoti ya mwaka wa fedha kuhusu bidhaa mbalimbali zilizokamatwa
na kuteketezwa kwa mujibu wa sheria na hatua zilizochukuliwa.
Mkurugenzi wa TFDA Hitti Sillo
amesema katika mwaka wa fedha wamekamata na kuteketeza vipodozi
ambavyo vimepigwa marufuku tani 16.61 ambazo thamani yake ni shilingi
milioni 44.2
.
.
‘Vipodozi
ambavyo vimepigwa marufuku vilivyoingizwa tumekamata vikiwa vinaingizwa
nchini na vingine vimekutwa katika soko vikiwa tayari vimeingizwa na
vingine vikiwa njiani kuingizwa nchini, mara nyingine tumekamata mabasi
yakiwa na vipodozi vinavyoingizwa nchini kinyume cha sheria vyote
hivyo thamani yake kwa mwaka wa fedha uliopita ni shilingi milioni 44″ Sillo.
Amesema kazi hiyo ni endelevu kwa kuwa
TFDA ipo sehemu mbalimbali nchini na wakaguzi wake wapo kuanzia
bandarini na katika viwanja vya ndege ambapo ndipo hukamataa bidhaa
nyingi.
Amesema miaka mitatu iliyopita udhibiti
umeimarika sana ndio maana matukio mengi ya kukamatwa kwa watu ambao
wanaingiza vipodozi hatari kinyume cha sheria wanakamatwa wakiwa
mipakani.
No comments:
Post a Comment