Saturday, 8 August 2015

Full time ya Chelsea vs Swansea City na matokeo mengine ya EPL nimeweka hapa

layiii
Baada ya Manchester United na Tottenham Hotspur kufungua dimba la mechi za ligi kuu ya Barclays Premier League – Mabingwa watetezi wa kombe hilo Chelsea nao jioni hii walianza utetezi wa kombe hilo kwa kucheza dhidi ya Swansea.
 
Mchezo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge umemalizika kwa sare ya 2-2.

  Oscar alianza kufungua ukurasa wa magoli katika dakika ya 23 kabla ya Andrew Ayew kusawazisha katika dakika ya 29. Dakika moja baadae Swansea walijifunga kupitia Fernandez aliyekuwa anataka kuokoa mpira uliopigwa na Willian.
  Dakika ya 55 Bafetimbi Gomez aliisawazishia Swansea baada ya golikipa Thibouit Courtois kupigwa red card na Gomez akafunga penati.
Matokeo Mengine ya BPL
 Man Utd 1-0 Spurs
Bournemouth 0-1 Aston Villa
Everton 2-2 Watford
Leicester 4-2 Sunderland
Norwich City 1-3 Crystal Palace

No comments:

Post a Comment

advertise here