Thursday 6 August 2015

HAWA NDIO WATU WABISHI NCHINI CHINA MTU WANGU

LAYIII

p>Ukijua sheria na haki yako ni rahisi kudai na kusimamia msimamo wako kiuhalali kabisa. Hali ndivyo ilivyo kwa wamiliki wa nyumba nyingi huko China ambao wengi ni wabishi hasa nyumba zao zinapotakiwa kubomolewa kupisha miradi mbalimbali.
Je hapa kwetu watu wanajua sheria na taratibu zao? Picha hapo chini zinaonyesha nchi ya kikomnisti ya China. Je nchi za kidemokrasia kama tunavyojiita unaweza kufanya hivi?
nail-house-china-2-v3

Mmiliki wa jengo hilo Luo Baogen, 67, akiwa na mkewe mwenye miaka 65 wamekuwa wakipambana kwa miaka minne ili waweze kupata dola za kimarekani 41,300 kutoka serikali kufidia jengo hilo ili waweze kuondoka hapo. Hali hiyo inaitwa nyumba misumari kwakuwa inakuwa ngumu
kumtoa kama hamjakubaliana naye na vile vile wana uwezo mkubwa wa kukuwajibisha kisheria.
nail-house-china-4

Nyumba msumari nyingine ikiwa katikati ya mtaa, kutokana na mwenye nyumba hiyo kushindwa kuafikiana na serikali kuhusu malipo ili iweze kubomolewa huko Nanning, Guangxi Zhuang.
nail-house-china-5
Ghorofa hili ambalo ni la mwisho kwenye eneo la mradi likiwa na bendera ya China huko jimbo la Henan. Inasemekana serikali ilishindwa kufikia muafaka na mwenye nyumba hiyo na hivyo amegoma kuondoka mahali hapo.
nail-house-china-7

Gharofa hilo ambalo ni hoteli likiwa katika eneo ambalo linatakiwa kujengwa soko kubwa la kibiashara katika wilaya ya Shenzhen. Mmiliki wa jengo hilo Choi Chu Cheung, na mkewe Zhang Lian-hao, wametaka kulipwa dola za kimarekani 2,327 kwa mita moja badala ya dola 840 kwa mita ambazo zilipendekezwa hapo kabla na wamiliki wa mradi.
nail-house-china-6

Na msumari huu mwingine ni katika eneo ambalo yanatakiwa kujengwa makazi mapya ya kisasa ya kuishi lakini mmiliki wake ametaka kulipwa fedha zaidi ndipo paweze kubomolewa, kulingana na vyombo vya habari vya huko china.
nail-house-china-1




No comments:

Post a Comment

advertise here