Monday, 31 August 2015

MTOTO WA MCHEZAJI BORA DUNIANI KUTOKEA BRAZIL AMENIUNGA NA CLUB YA URENO

LAYIII

Mtoto wa mchezaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Rivaldinho Rivaldo ambaye anafuata nyayo za baba yake Rivaldo katika soka, amesajiliwa na klabu ya Boavista ya
Ureno akitokea klabu ya Mogi Mirim ya kwao Brazil. Hivyo hiyo inakuwa mwanzo wa safari yake ya kusaka mafanikio kama aliyoyapata baba yake Ulaya.
ng887322E8-A487-4317-B9AD-945B6421D929
Rivaldinho ambaye ana umri wa miaka 20 amejiunga na klabu ya Boavista kwa mkataba wa miaka mitatu na kuhama katika klabu ambayo baba yake mzazi ni Rais, hiyo itamfanya kukua na kukomaa kisoka kwani ataanza kuishi mbali na uangalizi wa baba yake.
ng4618719
Mchezaji huyo ambaye amepata umaarufu kutokana na ukubwa wa jina la baba yake, ni kawaida kuingia katika headlines kila mara anapofunga goli, ameichezea klabu ya Mogi Mirim jumla ya mechi 44 na kufunga goli 10. Rivaldinho ili aweze kufikia rekodi za baba yake inabidi ajitume kwani hadi sasa hajawahi cheza katika timu ya taifa Brazil hata ya vijana.

No comments:

Post a Comment

advertise here