layiii
Taarifa hiyo imemazia kwa kuwataka Watanzania kumpuuza Dokta Slaa kwa kwakuwa ni miongoni mwanasiasa waliojaa uongo pamoja na upotoshaji wakupindukia
NA KAROLI
VINSENT
SIKU moja kupita baada ya aliyewai pata kuwa
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa
kumtuhumu mfanyabishara maarufu Afrika, Bilionea Rostam Azizi akidai kuwa
alimtishia maisha pamoja na kusema kuwa Mfanyabiashara huyo ndio anayeifadhili
Chadema kwenye Kampeni zinazoendelea nchini.
Hatimaye Bilionea huyo ameibuka na
kusema Doka Slaa ni muongo na mpotoshaji na anayee faa kupuuzwa.
Kwa mujibu
ya taarifa ya Rostam Azizi Iliyotolewa kwenye vyombo vya Habari nchini
inasema kuwa tuhuma anazotoa Dokta Slaa ni taarifa za uongo na
zilizojaa chuki binafsi na azipaswi kutolewa na Mtu anayesema ni
kiongozi wa kiroho
ambaye ni Padri,
Taarifa hiyo ya Azizi imesema kama Dokta
Slaa anahushahidi kwa hayo anayomtuhumu
atoe ushahidi hadharani, kwani asihishie kutoa uongo mbele za watu
akidai yeye Rostam hajawai kuifadhili chadema na wala hata kumtishia maisha
mwanasiasa huyo aliyekimbia siasa.
Amesema si kwa mara ya kwanza Dokta
Slaa kumtuhumu mfanyabiashara huyo mashuhuri Afrika mashariki na kati kwa
ujumla kwani amedai Slaa aliwai kumshutumu pia mwaka 2010 mara baada ya
kumalizika uchaguzi mkuu akisema Rais Jakaya Kikwete,Edward lowassa pamoja na yeye
Rostam Azizi kuwa walikutana kwenye hoteli moja jijini mwanza na kupanga
mikakati ya kumwibia kura zake.
Akidai siku hiyo anayosema Slaa
hakuwepo nchini bali alikuwepo nje ya nchi.
Taarifa hiyo imemazia kwa kuwataka Watanzania kumpuuza Dokta Slaa kwa kwakuwa ni miongoni mwanasiasa waliojaa uongo pamoja na upotoshaji wakupindukia
No comments:
Post a Comment