Monday, 31 August 2015

DAKTARI WA DIAMOND ATAFIA STUDIO

LAYIII
Musa Mateja na Gabriel Ng’osha
YAMEKUWA hayo! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ anahofiwa kufia studio kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kupumzika
jambo linalomsababishia ‘kuzima’ (kulala fofofo) mara kwa mara ndani ya studio.
diamond
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiuchapa usingizi studio.
Musa Mateja na Gabriel Ng’osha
YAMEKUWA hayo! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ anahofiwa kufia studio kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu pasipo kupumzika jambo linalomsababishia ‘kuzima’ (kulala fofofo) mara kwa mara ndani ya studio.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchana Diamond amekuwa akifanya kazi nyingi huku usiku akilazimika kuingia studio kwa ajili ya kuandaa nyimbo zake lakini hali hiyo sasa inaanza kuwa ngumu kwani mara kadhaa amekuwa akichoka na kujikuta akiuchapa usingizi mzito.
diamond studioCHANZO CHAZIDI KUMWAGIKA
Kikiendelea kuweka wazi, chanzo hicho kilisema hivi karibuni Diamond alitokewa na hali hiyo ya kulala akijitetea kwamba kabla ya kwenda studio alikuwa akitumbuiza kwenye shoo moja na baadaye usiku akatumbukia studio ili kurekodi lakini ilishindikana.
KISIKIE CHANZO
“Amekuwa na tabia ya kufanya kazi kupita kiasi na kujikuta akichoka hadi kulala usingizi wa fofofo.
“Siku moja akiwa kwenye Studio za THT (Dar) alichoka sana, akazima. Hali hiyo ilitushangaza sana kwani siku zote amekuwa akikesha akipiga mzigo wakati wengine wakiwa wamelala. Ila kwa hali hii mimi naona anatakiwa kuacha maana atakuja kupata matatizo makubwa,” kilisema chanzo hicho.
DAKTARI
Ijumaa Wikienda, juzi lilizungumza na daktari mmoja jijini Dar (aliomba hifadhi ya jina) ambapo alifafanua madhara yanayoweza kumpata msanii huyo kutokana na tatizo la kufanya kazi kupitiliza na kukosa muda wa kulala.
NI KINGA NA STAREHE
Kwa mujibu wa daktari huyo, watu wengi hawajui kuwa usingizi ni moja kati ya starehe nzuri na kubwa duniani. Lakini pia ni kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. Binadamu anaweza kufa ghafla, tatizo likianzia kwenye kukosa usingizi.
Daktari huyo alisema kwamba madhara ya kufanya kazi nyingi bila kupumzika ni mabaya sana kwani yanaweza kumfanya mtu apate athari nyingi.
“Ifahamike kuwa watu wengi duniani hawalali kwa wakati kutokana na mihangaiko ya maisha. Kwa kawaida binadamu anatakiwa alale saa 7-8. Asipofanya hivyo anaweza kupata athari kama shinikizo la moyo na akafa, ugonjwa wa kisukari, hasira za mara kwa mara, uwezo mdogo wa kufikiri, pia upungufu wa nguvu za kiume na kuzeeka haraka,” alisema daktari huyo.
Akaongeza: “Kwa hiyo namshauri huyo Diamond wenu, atenge muda wa kulala.”
AKUMBUSHWA YA WAKO JACKO
Daktari huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, hata kifo cha mfalme wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson ‘Wako Jacko’ kilichangiwa pia na uchovu wa kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika (aliwahi kukosa kulala kwa siku 60).
DIAMOND AFUNGUKA
Diamond alipoulizwa juu ya ishu hiyo alisema:
“Sina tatizo la kuzimia (ila anazima).
Ni kweli mara kadhaa nimekuwa nikifanya kazi ngumu sana kiasi cha kushindwakupumzika na mara kadhaa wasanii kibao tu huwa wanajikuta wakiuchapa usingizi mzito studio. Ila mimi baadaye huwanapiga mzigo kama kawaida,” alisema Diamond.


No comments:

Post a Comment

advertise here