Thursday 25 June 2015

BURUNDI KIMENUKA TENA

LAYIII
Wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu hatma ya uchaguzi mkuu wa Burundi unaotarajia kufanyika mwezi ujao kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea kupinga kugombea tena kwa Rais Pierre Nkurunziza..headlines zimerudi tena nchini humo.

Burundi tena kwenye headlines…inahusu kutoroka kwa makamu wa Rais!! kisa kiko hapa

vice
Wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu hatma ya uchaguzi mkuu wa Burundi unaotarajia kufanyika mwezi ujao kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea kupinga kugombea tena kwa Rais Pierre Nkurunziza..headlines zimerudi tena nchini humo.

burundi2
Makamu wa Rais wa nchini hiyo Gervais Rufikiri ametoroka nchini humo na kudaiwa kimbilia Ubelgiji  baada ya kupinga hatua ya Rais wa nchi hiyo kuwania muhula wa tatu akiungana na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na jaji mmoja wa mahakama ya kikatiba..
burundi
Licha ya msemaji wa serikali kukanusha madai hayo na kusema kuwa Rufikiri amesafiri nje kwa ziara rasmi ya kikazi lakini mwenyewe baada ya kuhojiwa na Televisheni ya France24 amesema ameondoka baada ya kuhofia maisha yake kufuatia kumpiga Rais huyo kuwania kwa muhula wa tatu ambapo ni kinyume na sheria.
Burundi imeingia katika mgogoro wa kisiasa tangu rais Nkurunziza atangaze nia ya kuwania muhula wa tatu kuongoza nchi hiyo huku maelfu ya watu wakikimbia nchi hiyo kwa kuhofia maisha yao.

No comments:

Post a Comment

advertise here