Wednesday, 31 May 2017

DAKTARI WA UPASUAJI MATITI AFUNGWA JELA MIAKA 15

 Daktari wa upasuajia wa matiti Ian Paterson amefungwa jela miaka 15 kwa kufanya upasuaji usio muhimu.

Paterson, mwenye umri wa miaka 59, aliwafanyia upasuaji wanawake tisa na mwanamume mmoja baada ya kuwadanganya kuwa walikuwa na saratani ya matiti.

Amepatikana na hatia ya mashtaka 17 ya kujeruhi kwa makusudi, baada ya kesi iliyodumu kwa mwezi mmoja uliopita.

Jopo la mahakama ya Nottingham liliambiwa kuwa Paterson alizidisha ama kubuni hatari ya saratani.

Mahakama iliambiwa kuwa alifanya upasuaji wa matiti kwa "sababu zisizojulikana" ambazo ni pamoja na shauku ya "kupata pesa za ziada".

No comments:

Post a Comment

advertise here