Thursday, 25 June 2015

baada ya mbrazil kusajiliwa liverpool sasa ni zamu ya mwingereza

layiii
Baada ya kufanikiwa kufanikisha usajili wa Danny Ings kutoka Burnley na Roberto Firmino kutoka Hoffenheim ya Ujerumani, klabu ya Liverpool sasa inatarajia kukamilisha usajili mchezaji mwingine ndaninya saa chache zijazo.

Baada ya Mbrazil Firmino, Liverpool sasa kumsajili beki huyu wa kiingereza

  Baada ya kufanikiwa kufanikisha usajili wa Danny Ings kutoka Burnley na Roberto Firmino kutoka Hoffenheim ya Ujerumani, klabu ya Liverpool sasa inatarajia kukamilisha usajili mchezaji mwingine
ndaninya saa chache zijazo.
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya England, Liverpool wamefanikiwa kutuma ofa iliyokubaliwa na Southampton kwa ajili ya kumsaini beki wa kimataifa wa England – Nathaniel Clyne.
Liverpool walituma ofa ya £12.5million kwa ajili ya Clyne, na baada ya Southampton kuikubali sasa kilichobaki ni suala la vipimo vya afya ili mchezaji huyo ajiunge nao.
Clyne ambaye yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Southampton kwa sasa yupo mapumzikoni na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka 5 ikiwa atafuzu vipimo vya afya.
Roberto Firmino baada ya kusaini Liverpool
Mchezaji huyu anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool katika dirisha hili la usajili, akiungana na Firmino aliyetua Anfield kwa ada ya £29m. Wachezaji wengine waliosajiliwa ni James Milner, Adam Bogdan na Charlton’s Joe Gomez

 


No comments:

Post a Comment

advertise here