UNGANA NA LAYIII
Afrika Kusini imesema kuwa huenda ikajiondoa kutoka kwa mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC yenye makao yake makuu huko Hague
Uholanzi kufuatia jaribio la kumkamata rais wa Sudan Omar al Bashir
alipokuwa nchini humo majuzi.
Afrika Kusini huenda ikajiondoa kwenye ICC
Afrika Kusini imesema kuwa huenda
ikajiondoa kutoka kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC
yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi kufuatia jaribio la kumkamata
rais wa Sudan Omar al Bashir alipokuwa nchini humo majuzi.
Hata
hivyo Nusra akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu
uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Lakini
baada ya kikao maalum cha baraza la mawaziri nchini humo, serikali
ilitoa onyo kuwa huenda ikalazimika kujiondoa kutoka kwa makubaliano
yeyote na mahakama ya ICC kutokana na sababu kadha.
''Serikali inawajibu wake wa kimataifa lakini pia inawajibu wake kisiasa''taarifa hiyo ilisema.
''iwapo
hatutakuwa na suluhisho maalum itakayotusaidia kutanzua taharuki
iliyopo kwa sasa nafikiri serikali yetu haitakuwa na budi ila kujiondoa
kutokana na makubaliano yeyote na ICC''iliendelea kusema.
Mahakama
ya Afrika Kusini ilikuwa imemuagiza rais Bashir kusalia nchini humo
huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo la kukamatwa kwake
litekelezwe au la.
Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake rais Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurejea nyumbani.
Rais Bashir alipokewa kwa shangwe na nderemo aliporejea Khartoum
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa
viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba
ilihitajika kumkamata kwa kuwa ni mwanachama wa ICC.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado zipo.
Rais
al Bashir anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na
uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi
inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.
No comments:
Post a Comment