LAYIII
Ni TBT!! Throwing back thursday ambapo huwa tunaitumia hii siku kushare
zile picha zetu za zamani ambapo kwenye millardayo.com kila wiki tutakua
tunakuletea picha mbalimbali za mastaa wakiwa kwenye pozi miaka kadhaa
iliyopita.
TBT: Picha 5 za zamani za Jokate, Wema Sepetu na ya Q Chief na Diamond, Millard Ayo na JK na Lowassa
Mwigizaji Wema Sepetu na Marehemu Kanumba.
Ni TBT!! Throwing back thursday ambapo huwa tunaitumia hii siku
kushare zile picha zetu za zamani ambapo kwenye millardayo.com kila wiki
tutakua tunakuletea picha mbalimbali za mastaa wakiwa kwenye pozi miaka
kadhaa iliyopita.
Q Chief na Diamond Platnumz.
Mrembo Jokate Mwegelo kwenye udogo wake.
Ni gazeti la Nipashe June 13 1995, hii picha nimeitoa kwenye Instagram page ya Dr. Cheni.
Mtu wako wa nguvu Millard Ayo enzi hizo
Lowassa wakiwa na kikwete enzi hizo
Taarifa
kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, huenda akaenguliwa iwapo
atatangaza nia na kuchukua fomu kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, zimezidi kushika kasi. Lowassa
hajatangaza kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa katika utumishi wa umma
nchini, lakini harakati zake za siasa pamoja na watu wake wa karibu
zinaonesha kuwa Mbunge huyo wa Monduli kwa zaidi ya miaka 20, huenda
akawa mgombea. Umeundwa
pia mtandao unaosambaza taarifa kuwa Lowassa anaumwa, ukitaraji kuwa
umma utafika mahala utaamini maneno hayo, ambayo yamesemwa mara kadhaa,
na Lowassa akajitokeza hadharani akiwa mwenye siha njema. Mmoja
wa viongozi wa CCM, ameieleza JAMHURI kwamba Mwenyekiti wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete, yuko njiapanda kutokana na shinikizo la kuchuja wagombea
Aprili, mwaka huu akiwamo Lowassa. Mtoa
taarifa amesema hatari kubwa iko kwa vigogo watatu ambao baadhi yao
wametangaza nia. Vigogo au makada hao kwa sasa wanapigiwa chapuo waingie
hatua ya tatu bora ndani ya CCM, na hapo ndipo wanapopambana Lowassa
asifikie. Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye tayari ametangaza ‘kimyakimya’, nao
wanatajwa kumtesa Rais Kikwete. “Hili
linamuumiza kichwa Mwenyekiti (Rais Kikwete). Kwa kweli yuko njiapanda.
Watu anaofanya nao kazi anawatosaje? Yeye mwenyewe halisemi hili ovyo.
Ni gumu na linalosumbua kichwa,” anasema mtoa habari na kuongeza. “Kuna
mashinikizo ya kuwafikiria anaofanya nao kazi kwa sasa, Makamu wa Rais
amefanya naye kazi kwa kipindi chote cha miaka mitano; Waziri Mkuu
atamtosa vipi, rafiki yake Membe atamtoa vipi?” anahoji mtoa taarifa. “Hawa
ni lazima wapite, kwa sababu taarifa zinasema kama Lowassa akipenya tu
ndani ya tatu bora, ujue atateuliwa. Mbinu hapa ni kufanya asifike
huko,” anasema mtoa taarifa huyo aliyeomba kuhifadhiwa jina. Lowassa
hajatangaza kuwania nafasi hiyo, ila karibu kila kona ya nchi hii
mazungumzo ya wananchi wa kawaida wanasema wazi kuwa wangetaka Lowassa
apewe usukani aweze kunyoosha mambo yaliyopinda kutokana na falsafa yake
ya kufanya uamuzi mgumu kwa wakati bila kuremba. Bernard
Membe kwa upande wake, ingawa ametangaza tayari kutogombea ubunge
katika Jimbo la Mtama, ambapo Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape
Nnauye, amejipanga kugombea jimbo hilo, kuhusu urais, anasema hadi sasa
“hajaoteshwa.” Makamu
wa Rais, Dk. Bilal mwishoni mwa mwaka jana wakati Rais Kikwete anaumwa
alikutana na wahariri kwa chakula cha jioni nyumbani kwake, na wahariri
walipomhoji iwapo atagombea urais, maana wakati huo alikuwa Kaimu Rais,
Rais Kikwete alipokuwa Marekani kwa matibabu, wasaidizi wake walijibu
kwa niaba yake kuwa hawajasikia neno la aina hiyo kutoka kwake. Yeye
hakujibu neno hilo, badala yake akapiga picha na wahariri
wakatawanyika. Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, yeye alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la
Uingereza (BBC) iwapo ana nia ya kugombea urais, alimjibu Salim Kikeke,
ambaye ni Mtangazaji wa BBC kuwa yeye bado anatangaza “kimyakimya.” Mbinu
nyingine inayopendekezwa kutumiwa kukata jina la Lowassa ni kuendelezwa
kwa adhabu dhidi ya kada huyo pamoja na makada wengine watano ambao
mwaka mmoja uliopita, waliadhibiwa na chama kutokana na kasi ya kuonesha
nia ya kuwania urais. Makada
wengine walioadhibiwa na Lowassa ni Membe, Waziri Mkuu mstaafu,
Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), Stephen
Wasira, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, na
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja. Licha
ya makada hao kufungiwa mwaka mmoja kuanzia Februari 18, mwaka jana
kutojishughulisha na shughuli za kisiasa kwa kuwa zingewapa kura ya
turufu katika kuwania uongozi wa nchi, baadhi yao hawakujali kwani
waliendelea kutangazani nia. Viongozi
hao waliadhibiwa na Kamati Ndogo Maalum ya Nidhamu iliyowatia hatiani
kwa kosa la kuanza kampeni mapema. Kamati hiyo iliongozwa na Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula. Hata
hivyo, Makamba, Wasira na Sumaye wameendelea na shughuli za kijamii
bila hofu, huku wengine wakijitokeza akiwamo Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba; Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Asiye na Wizara Maalum, Profesa Mark
Mwandosya, na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla. Mtoa
taarifa anasema tahadhari kubwa ya Rais Kikwete ipo katika kutengeneza
uhusiano na diplomasia ndani ya chama kwamba baada ya uteuzi kusiwe na
mgawanyiko aina yoyote. Mtoa
habari ambaye ametoka kwenye vikao vya CCM huko Zanzibar amesema kwa
nia ya kujenga uaminifu kwenye chama na Serikali, anasema Rais Kikwete
anapata taabu kutokana na Lowassa kuwa na sifa mbili kwake. Kwanza
Rais Kikwete anawaza uhusiano kati yake na Lowassa walioutangaza kwamba
“hawakukutana barabarani”, na pili nguvu ya ushawishi na Lowassa
kuungwa mkono na wanachama wengi na hata nje ya chama. Licha ya Lowassa
kutotangaza nia, lakini waliotangaza nia, kauli zao zinaonesha kutaka
kupambana na mbunge huyo ambaye CCM ilifikia hatua ya kumpunguza kasi
yeye na makada wenzake watano mwaka jana. Taarifa
zinasema kwa mara ya kwanza wakati Rais Kikwete anaingia madarakani,
alikubali kupewa Makamu Rais aliyekuwa Mgombea Mwenza, Dk. Mohamed Shein
lakini akapinga kuletewa Waziri Mkuu. Nafasi hiyo alimpa kada mwenzake
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge wa Monduli Lowassa ambaye
alikitumikia cheo hicho kwa miaka miwili na mwezi mmoja kabla ya
kujiuzulu akateuliwa Pinda. Abdulrahman
Kinana, Katibu Mkuu wa CCM ameiambia JAMHURI kuwa chama hakina mpango
wa kumtimua mwanachama yeyote kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo
vya habari. Lakini
akasisitiza, “CCM itakuwa makini sana na mgombea atakayeteuliwa. Katika
hili la urais na uchaguzi wa wabunge na madiwani, chama kiko makini
sana katika haya. Sawa.” Mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM unatarajiwa
kukamilishwa Aprili, mwaka huu. Hii ina maana mwezi Machi utakuwa mwezi
wa mikikimikiki. Wagombea watarajiwa karibu wote hawakuwa tayari
kulizungumzia hili, wakiiambia JAMHURI kuwa wakati haujawadia
No comments:
Post a Comment