Thursday, 7 April 2016

MUIMBAJI MAARUFU AFARIKI JUKWAANI

LAYIII
 
Huzuni na mshangao umeghubika Indonesia baada ya muimbaji maarufu Irma Bule, aliyekuwa akiwatumbuiza mashabiki wake kuanguka na kufariki dunia jukwaani
Yamkini bi Bule aliumwa na nyoka yapata dakika 45 zilizotangulia katika ''shoo yake'' iliyokuwa magharibi mwa Java Indonesia.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya ''shoo'' yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.
Japo nyoka huyo alikuwa ameng'olewa chonge zake , kwa njia moja au nyingine aliweza kum'gata na
kuingiza sumu ndani ya damu yake.
Duru zinasema kuwa alipewa dawa ya kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.
Aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake wakang'amua hali haikuwa nzuri.
Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.
Walipomkimbiza hospitalini daktari aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.

No comments:

Post a Comment

advertise here