Thursday, 7 April 2016

MTOTO WA DARASA LA TANO AKUTWA KAJINYONGA

LAYIII
ccccccccccccccc-zDada wa marehemu akilia baada ya mdogo wake kujinyonga.
STORI: Dustan Shekidele, Wikienda
Morogoro: Mshtuko! Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake, Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.

Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi nyumbani kwao maeneo ya Mji Mpya mjini hapa.
DSC_5576Kitenge cha mama yake alichotumia kujinyongea.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.
DSC_5584Mama mzazi akilia kwa uchungu.
“Anosisye alichelewa kurudi nyumbani, ilipofika saa 4:00 usiku, mama yake aliamua kumtafuta akaambiwa alionekana akiwa na lile kundi lililokupora wewe (mwandishi wetu) maeneo ya Stendi ya Daladala ya Mji Mpya,” alisema mmoja wa mashuhuda hao huku akirekodiwa.
DSC_5579Mashuhuda wakifuatilia tukio hilo.
Kwa upande wake, mama mzazi wa denti huyo aliyeangushiwa zigo la lawama juu ya kifo cha mwanaye alisema: “Mwanangu alichelewa kurudi nyumbani usiku. Nilizunguka kumtafuta, nikaambiwa alionekana akiwa na Kizazi Jeuri hivyo nilimchapa sana na kumtisha kukicha nitampeleka polisi.
“Kulipokucha aliandaa nguo za shule, cha ajabu nimemkuta amejinyonga. Inauma sana jamani.”
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  wa Makaburi B, Amiri Kombo aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake.
DSC_5591Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwaajili ya uchunguzi.
Wazazi wanahofia watoto wao kujiunga na kundi hilo lililomvamia mwandishi wetu na kumpora kamera na simu ambao aliwafungulia jalada la kesi namba MOR\RB\140\2016 hivyo wanasakwa na polisi.

No comments:

Post a Comment

advertise here