Wednesday, 6 April 2016

MAMBA WA AJABU AUWAWA HUKO FROLIDA

LAYIII
CHANZO na bbc swahili
unaweza bonyeza picha kujiunga nami habari kwa njia ya video
Lightseyh
Mamba mkubwa mla ng’ombe ameuawa katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Mnyama huyo alikuwa na uzani wa kilo 360.
Mwindaji Lee Lightsey amesema mamba huyo wa ukubwa wa futi 15 (4.5m) ndiye mkubwa zaidi ambaye amekumbana naye katika kipindi cha miaka 18.
Baada ya kumuua, alihitaji trekta kumbeba.
Bw Lightsey alimgundua mnyama huyo akiwa na mwelekezi wa wawindaji Blake Godwin walipokuwa
katika maeneo ya kumnyweshea mifugo maji Jumamosi.
Walimfyatulia risasi mamba huyo alipokuwa umbali wa mita sita kutoka kwao.
"Ingawa mnyama huyu ni mnene hivi, sijashangaa kwamba amekuwepo,” amesema Bw Lightsey.
“Tumewapata wengi ambao wamekuwa wadogo kiasi tu kumshinda katika miaka 20 ambayo tumekuwa tukiwinda.
"Kilichotuvutia ni kwamba anaonekana amekuwa akiwala ng’ombe wetu, kwa sababu tulipata vipande vya nyama majini. Alikuwa dubwana lililostahili kuangamizwa.”
Bw Lightsey anasema mamba mkubwa zaidi ambaye amewahi kumuua alikuwa na urefu wa futi 13ft (4m).
Mamba
Mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Indonesia amependekeza mamba watumiwe kulinda wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.
Budi Waseso anataka taifa hilo lijenge gereza kwenye kisiwa na kizingirwe na mamba akisema wanyama hao ni walinzi bora kushinda wanadamu, kwani hawawezi kuhongwa.
Amesema atazuru maeneo mbalimbali katika taifa hilo kutafuta mamba wakali zaidi.
Indonesia ina moja ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya duniani na ilianza tena kunyonga watu baada ya kusitisha hukumu hiyo kwa miaka mine 2013.
"Tutaweka mamba wengi sana huko,” Bw Waseso alinukuliwa na tovuti moja nchini humo kwa jina Tempo.
"Huwezi kuwahonga mamba. Huwezi kuwashawishi waruhusu washukiwa watoroke.”
Mpango huu bado umo katika hatua za mwanzo mwanzo nab ado haijaamuliwa gereza hilo litakuwa wapi na ni lini litafunguliwa, shirika la habari la AFP limesema.



No comments:

Post a Comment

advertise here