Duniani
kote wataalamu wanaangalia namna ya kubuni teknolojia itakayosaidia
kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa, mpshi wa viwanda,
magari vinatajwa kama vyanzo vya
tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.
Jaribio linafanywa sasa hivi
likifanikiwa basi huenda historia ikaingia kwenye ukurasa mwingine,
ndege inayotumia umeme wa nguvu ya jua imeanza safari ambapo tayari
imeruka kutoka Abu Dhabi.
Ndege hiyo ina kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa kama wa ndege ya kawaida na uzito sawa na gari, mabawa yake yana solar panels ambazo zinasaidia kunasa nishati ya mwanga wa jua.
Ndege hiyo ina betri zinazohifadhi nguvu ya umeme wa jua kutoka kwenye jua na hivyo itaweza kusafiri hata usiku, Andre Borschberg ndio
rubani anayerusha ndege hiyo katika safari ya miezi mitano kuizunguka
dunia, ambapo inakadiriwa umbali atakaosafiri ni zaidi ya Kilometre
35,000.
Ndege hiyo inasafiri na ujumbe wa
kuhimiza uwekezaji kwenye Teknolojia salama ambayo ni rafiki kwa
mazingira na ikifanikiwa kumaliza safari yake itaingia kwenye rekodi za
kuwa ndege ya kwanza inayotumia nishati ya jua kusafiri duniani.
No comments:
Post a Comment