Watafiti
wamekuwa wakigundua baadhi ya viumbe kutumika sehemu mbalimbali,
tumeona panya wanaotegua mabomu,
Watafiti wa magonjwa ya Cancer
Uingereza wanasema kuwa mbwa ana kitu cha ziada muhimu kwenye afya ya
binadamu.
Utafiti
wa wataalamu hao unaonesha mbwa anaweza kugundua saratani ya Tezi ya
shingo ya binadamu (Thyroid) kwa kunusa tu, ambapo katika majaribio
waliyofanya imeonekana 88% ya watu waliogundulika na mbwa walionekana
kuwa na saratani hiyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.
Mbwa aina ya frankie kutoka
Ujerumani alifundishwa kunusa mikojo ya watu wenye ugonjwa huo na majibu
kuonesha kuna asilimia kubwa mbwa huyo anaweza kugundua watu
walioathirika na cancer hiyo.
Wanasayansi wanaona kwa hii njia mpya huenda ikayasaidia maeneo mbalimbali duniani ambayo hayana vifaa vya kupimia ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment