Monday, 9 March 2015

MATUMIZI MABAYA YA 911 YAMPONZA

922Ndani ya wiki hii headlines kuhusu Marekani na ishu ya dawa za kulevya ni sehemu tu ya zile nyingi zilizotufikia,
idadi ya majimbo ambayo wamehalalisha matumizi ya bangi inatarajiwa kuongezeka muda wowote, leo nna hii ya jamaa ambaye alijikuta akijikabidhi mwenyewe Polisi kwa kesi ya dawa za kulevya aina ya cocaine.
Kutoka Ohio kuna story ya jamaa aliyepiga simu Polisi kuripoti kwamba mkewe amemuibiwa dawa hizo za kulevya, Polisi wakamkata na kumfikisha Mahakamani.
Jamaa huyo  Robert D. Collins ambaye umri wake ni miaka 39 alishtakiwa kwa makosa mawili, kwanza kwa matumizi mabaya ya namba ya dharura ya 911 na pia kukutwa na kiko ambayo ndani yake ilikutwa na bangi japo haikufahamika kama mke wake alikutwa na cocaine ambazo Collins alilalamika kuibiwa.

No comments:

Post a Comment

advertise here