Kwetu TZ kuikuta bidhaa
kutoka China kwenye duka lolote sio kitu cha kushangaza kiukweli, kuna
radio, simu, TV na bidhaa nyingine nyingi sana ambazo tunazinunua na
kutumia ambazo zina maandishi ‘Made in China‘.
Kwa Marekani kumbe kuna bidhaa ikiingia
kwenye soko lao ikiwa imetengenezwa China ni ishu ambapo inafanya kuwa
habari kubwa kwa upande mwingine.
Joshua Slocum
ni mmiliki wa kampuni ambayo inatoa huduma za mazishi anasema mfumo wa
Marekani kuruhusu watu ambao wamewekeza kwenye huduma kama ya Kampuni
yake kuingiza bidhaa toka nje ni kitu ambacho Serikali imeweka utaratibu
mgumu sana ili kuzuia biashara hiyo.
Slocum anasema bei ya
jeneza moja Marekani ni kama dola 2000 (zaidi ya Mil. 3 na nusu Tshs)
wakati jeneza moja toka China ni kama dola 350 tu (sawa na laki 6 Tshs),
lakini Serikali imezuia kabisa kuingizwa kwa majeneza toka China,
wakati matumizi yake ni yaleyale na hata ubora na kiwango chake pia.
Jamaa anasema Hillenbrand, Matthews International, and Aurora Casket ndio
makampuni makubwa yanayouza majeneza Marekani, wanajipangia bei na
utaratibu pia wa kufanya biashara yao kitu ambacho kwa watu wa kipato
cha chini wanapata wakati mgumu kumudu gharama za majeneza wakipata
msiba.
Slocum hapendezwi na
utaratibu huo, anasema wote tutakufa haijalishi umezikwa au umechomwa
moto.. Jeneza sio kitu kitakachobadili kitu chochote; “We
all go back to the earth. I don’t care whether you’re cremated, whether
you’re buried in a sealed American casket or a non-sealed casket,
there’s no funeral product on earth that will make you any less dead“– Joshua Slocum.
No comments:
Post a Comment