Monday, 9 March 2015

INACHEKESHA KWELI ETI WEMA NAYE KAWA MBOGO TEHE TEHE

Stori: Imelda Mtema/ijumaawikienda
STAA wa sinema asiyekaukiwa matukio Bongo, Wema Sepetu amezua kioja cha aina yake baada ya kutajiwa jina la aliyekuwa mwandani wake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Staa wa sinema asiyekaukiwa matukio Bongo, Wema Sepetu.
Kioja hicho alikifanya juzikati nyumbani kwake, Kijitonyama jiji Dar alipokuwa akirekodi kipindi chake cha In My Shoes ndipo aliposhtuka baada kutumiwa maoni na moja wa shabiki wake kupitia mtandao wa simu.“Heeeh! Huyu vipi tena ananitajia jina hili (Diamond)? Sitaki kabisa kulisikia, hapa nataka kusikia mimi na maisha yangu na si maisha ya mtu mwingine,” alisikika Wema.

No comments:

Post a Comment

advertise here