Ibrahimu Mussa na Khadija Mngwai, Dar es Salaam
MASHABIKI wa Yanga na Simba jana almanusura wazichape uwanjani, baada ya mashabiki wa Simba, Tawi la Karume kuingia uwanjani na mfano wa
jeneza ambalo lilikuwa limeandikwa jina la nyota wa Yanga, Amissi Tambwe, hali iliyowaudhi mashabiki wa Yanga, Tawi la Ukombozi Keko waliowavaa na kuwatimua na jeneza lao.
Tukio hilo lilijiri katika mchezo baina ya Simba na Yanga uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mashabiki wa Simba waliingia kwa staili ya aina yake ya kushangilia huku wakimkebehi Tambwe ambaye alitokea Simba kujiunga na Yanga.
Kimbwaga zaidi ni kwamba walikuwa wameandika jina la Tambwe huku wakiwa wamevalia jezi namba 19, ambayo anaivaa kwenye kikosi cha Yanga.
Katika hatua nyingine, kundi la wanachama lililofutwa uanachama, Simba Ukawa, liliwatimua mashabiki wa Tawi la Karume waliotaka kukaa jukwaa lao na kuamua kujitenga.

No comments:
Post a Comment