Wednesday, 15 February 2017
MANENO YA KIKWETE KUHUSIANA NA SWALA LA MADAWA YA KULEVYA
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete, amefunguka kuhusu sakata la dawa za kulevya na kuipongeza serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.
Kikwete amefunguka hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, kinachoruka kila siku saa 11:00 alfajiri hadi saa 3:00 asubuhi.
Kikwete amefunguka hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, kinachoruka kila siku saa 11:00 alfajiri hadi saa 3:00 asubuhi.
DIVA AFUNGUKA KUHUSU KUTAMANI KUDATE NA ALIKIBA
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady
amefunguka kwa kudai kuwa katika mastaa wa muziki Alikiba ndiye msanii
ambaye anatamani kudate naye.
Diva ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji Heri Muziki, alikuwa
host wa show ya Valentine’s Day iliyofanyika Jumatano hii katika ukumbi
wa Next Door na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali.
Akiongea na waandishi kabla ya kwenda kusherehesha show hiyo
iliyoandaliwa na Irene Uwoya, Diva alidai Alikiba ndiye msanii ambaye
anatamani kudate naye.
BREAKING NEWS: MASOGANGE NDANI KWA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA
TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo,
anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu
Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central)
akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba,
mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye
orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo,
HAKIMU NA KARANI KIZIMBANI KWA RUSHWA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mara
imewapandisha kizimbani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mjini Musoma,
Swalala Mathayo (40) na karani wa Mahakama hiyo, Charles Masatu (56) kwa
tuhuma za kudai na kupokea rushwa.
Tuesday, 14 February 2017
MAAJABU: MIMBA MIEZI 13 AJIFUNGUA CHUA NA MDUDU MWENYE MANYOA MEUSI
Na Ibrahim Yassin, Kyela
MKAZI wa Kitongoji cha Njisi, Kijijiji cha Kilwa, wilayani Kyela, Tummanye Makula (35) , amekaa na ujauzito miezi 13 na kushindwa kujifungua.
Hata hivyo, baada ya maombezi, alijikuta akijifungua chura na baadaye mdudu wa ajabu akiwa na manyoya meusi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya dada huyo kumpigia simu Mchungaji wa Kanisa la Tample Of Prayer For All Nations Church, Nabii Charles Mkuvasa wa mjini Kyela akihitaji kuombewa.
Alicuhukua hatua hiyo baada ya kukaa na ujauzito kwa muda wote huo na kushindwa kujifungua, licha ya
AMUUA MFANYAKAZI WA SHAMBA AKIZANI NI MNYAMA NGIRI
Stephen Hepburn alifikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya mauaji.
Yeye na mwenzake wa kike walikuwa wakiwawinda ngiri kwenye shamba moja lililo mkoa wa Limpopo kaskazini siku ya Jumamosi, wakati Jan Railo ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 aliuawa.
VIDEO: ALIKOLAZWA MANJI ULINZI NI WA KUFA MTU HUKO MUHIMBILI TAASISI YA MOYO
Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.
Manji aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa alipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.
Askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa mwenyekiti huyo wa
Monday, 13 February 2017
AC MILAN WAPANGA MIPANGO KWA SANCHEZ, LUKAKU
Klabu ya AC Milan imeripotiwa kuwa katika harakati za kutaka kuwasajili washambuliaji wanaocheza katika ligi ya nchini England Romelu Lukaku wa Everton pamoja na Alexis Sanchez wa Arsenal.
Wawili hao wanatajwa kuwa kwenye mipango ya klabu hiyo ya mjini Milan, itakapofika mwishoni mwa msimu huu, na tayari imearifiwa fungu la pesa limetengwa kwa ajili ya uhamisho wao.
DKT. SLAA AMTUMIA UJUMBE GWAJIMA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA
Vita ya kupambana na dawa za kulevya nchini iliyopamba moto zaidi na kuzua mijadala tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipoanza kutaja majina ya watuhumiwa imemuibua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa.
Dkt. Slaa ameibuka baada ya kutajwa na kuhojiwa kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye alikuwa rafiki yake na ‘muwezeshaji’ wake kabla siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hazijawageuza kuwa mahasimu.
Sunday, 12 February 2017
NAPE APIGA ‘STOP’ ZUIO LA TCRA KUHUSU TV ZA MTANDAONI
Siku chache baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudaiwa kuzuia uendeshaji wa runinga za mtandaoni (online TV), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametengua zuio hilo.
Nnape ameeleza kuwa ameamua kusimamisha zuio hilo kwakuwa halitakuwa na tija kwa wakati huu kwani kanuni zinazotoa muongozo wa namna ya kuendesha maudhui ya mtandaoni bado ziko kwenye
WATUHUMIWA 16 WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MKOANI KAGERA
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi Tanzania,Magereza na uhamiaji wilaya ya Karagwe mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa wa madawa ya kulevya 16 wakiwemo watendaji wa serikali za vijiji wanaojihusisha na biashara haramu katika mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda kinyume cha sheria za nchi.
PAUL MAKONDA AFUNGUKA KUHUSU KUHOJIWA NA BUNGE
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kwa kuwa hajapokea barua ya kuitwa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema hatoweza kwenda mbele ya kamati hiyo bila barua rasmi iliyomtaka kufanya hivyo.
Bunge lililokuwa likiendelea na vikao vyake Dodoma kabla ya kuahirishwa juzi, lilipitisha uamuzi wa kuwataka Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alaxander Mnyeti, kufika mbele ya kamati hiyo na kuhojiwa kutokana na kauli walizozitoa, zinazodaiwa kuudharau mhimili huo wa dola.
Saturday, 11 February 2017
KAMISHNA MPYA DAWA ZA KULEVYA AFUNGUKA


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Rogers Sianga kuwa kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).
Baada ya kuteuliwa Sianga alizungumza na Mwananchi na kusema kwanza anamshukuru Mungu kwa uteuzi huo na akaahidi kushughulikia kwa karibu kesi za vinara wa ‘unga’.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais jana, Gerson Msigwa ilisema Sianga atasaidiwa na Mihayo Msikela atakayekuwa Kamishna wa Operesheni na Fredrick Kibuta atakayekuwa Kamishna wa Intelijensia.
Uteuzi huo umekuja siku chache baada ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) kumtaka
SPIKA WA BUNGE AKEMEA TABIA YA WABUNGE KUKAMATWA KIBABE BUNGENI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amekemea tabia ya ukamatwaji wa wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na kusema kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu.
Akihitimisha mkutano wa sita wa Bunge, Ndugai amesema kama kuna kiongozi yeyote wa serikali anamuhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala ya kwenda
Friday, 10 February 2017
MENGINE YAIBUKA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kujiridhisha na kiwango cha mapato linayokusanya kwa usafirishaji mizigo iwapo kiko sahihi.
Majaliwa amesema hayo alipotembelea makao makuu ya ATCL jijini Dar es Salaam kujionea utendaji tangu lilipoboreshwa mwaka jana kwa kununuliwa na Serikali ndege mpya mbili.
Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga kuhakikisha anatekeleza suala hilo.
Pia, ametakaka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba za njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
Vievile amesema ataagiza uchunguzi ufanywe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) utakaolenga kujua ukusanyaji mapato katika kipindi hicho.
Waziri Mkuu akasema Serikali haitakuwa tayari kushuhudia shirika hilo linakufa tena na kuwataka viongozi wahakikishe linaendeshwa kwa faida kwa manufaa ya Taifa.
MAJIBU YA MAALIM SEIF BAADA YA PROF LIPUMBA KUMTAKA WAYAMALIZE
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Maalim Seif alitoa kauli hiyo kwenye ziara ya siku nne kwenye wilaya saba za mikoa mitatu ya Unguja.
Maalim alisema ataendelea kufuata taratibu za kisheria ili kuhakikisha chama kinamaliza moja kwa moja mgogoro aliodai umepandikizwa na CCM kupitia kwa Lipumba.
Subscribe to:
Posts (Atom)