Monday, 13 February 2017

AC MILAN WAPANGA MIPANGO KWA SANCHEZ, LUKAKU



Klabu ya AC Milan imeripotiwa kuwa katika harakati za kutaka kuwasajili washambuliaji wanaocheza katika ligi ya nchini England Romelu Lukaku wa Everton pamoja na Alexis Sanchez wa Arsenal.
Wawili hao wanatajwa kuwa kwenye mipango ya klabu hiyo ya mjini Milan, itakapofika mwishoni mwa msimu huu, na tayari imearifiwa fungu la pesa limetengwa kwa ajili ya uhamisho wao.

DKT. SLAA AMTUMIA UJUMBE GWAJIMA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA



Vita ya kupambana na dawa za kulevya nchini iliyopamba moto zaidi na kuzua mijadala tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipoanza kutaja majina ya watuhumiwa imemuibua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa.
Dkt. Slaa ameibuka baada ya kutajwa na kuhojiwa kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye alikuwa rafiki yake na ‘muwezeshaji’ wake kabla siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hazijawageuza kuwa mahasimu.

Sunday, 12 February 2017

NAPE APIGA ‘STOP’ ZUIO LA TCRA KUHUSU TV ZA MTANDAONI




Siku chache baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudaiwa kuzuia uendeshaji wa runinga za mtandaoni (online TV), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametengua zuio hilo.
Nnape ameeleza kuwa ameamua kusimamisha zuio hilo kwakuwa halitakuwa na tija kwa wakati huu kwani kanuni zinazotoa muongozo wa namna ya kuendesha maudhui ya mtandaoni bado ziko kwenye

KWA NJIA HIZI PESA HAZITAKUKWEPA KAMWE

IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima

WATUHUMIWA 16 WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MKOANI KAGERA



Jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi Tanzania,Magereza na uhamiaji wilaya ya Karagwe mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa wa madawa ya kulevya 16 wakiwemo watendaji wa serikali za vijiji wanaojihusisha na biashara haramu katika mpaka wa Tanzania na nchi ya Rwanda kinyume cha sheria za nchi.

PAUL MAKONDA AFUNGUKA KUHUSU KUHOJIWA NA BUNGE



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kwa kuwa hajapokea barua ya kuitwa.

Akizungumza  jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema hatoweza kwenda mbele ya kamati hiyo bila barua rasmi iliyomtaka kufanya hivyo.

Bunge lililokuwa likiendelea na vikao vyake Dodoma kabla ya kuahirishwa juzi, lilipitisha uamuzi wa kuwataka Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alaxander Mnyeti, kufika mbele ya kamati hiyo na kuhojiwa kutokana na kauli walizozitoa, zinazodaiwa kuudharau mhimili huo wa dola.

Saturday, 11 February 2017

HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA GWAJIMA BAADA YA KUTOKA KITUO CHA POLISI



Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima ameachiwa na Polisi leo jioni baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi mchana kwenye kituo

KAMISHNA MPYA DAWA ZA KULEVYA AFUNGUKA




Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Rogers Sianga kuwa kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Baada ya kuteuliwa Sianga alizungumza na Mwananchi na kusema kwanza anamshukuru Mungu kwa uteuzi huo na akaahidi kushughulikia kwa karibu kesi za vinara wa ‘unga’.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais jana, Gerson Msigwa ilisema Sianga atasaidiwa na Mihayo Msikela atakayekuwa Kamishna wa Operesheni na Fredrick Kibuta atakayekuwa Kamishna wa Intelijensia.

Uteuzi huo umekuja siku chache baada ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) kumtaka

SPIKA WA BUNGE AKEMEA TABIA YA WABUNGE KUKAMATWA KIBABE BUNGENI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amekemea tabia ya ukamatwaji wa wabunge wanapokuwa kwenye vikao vya Bunge na kusema kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu.


Akihitimisha mkutano wa sita wa Bunge, Ndugai amesema kama kuna kiongozi yeyote wa serikali anamuhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala ya kwenda

Friday, 10 February 2017

MENGINE YAIBUKA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kujiridhisha na kiwango cha mapato linayokusanya kwa usafirishaji mizigo iwapo kiko sahihi.

Majaliwa amesema hayo alipotembelea makao makuu ya ATCL jijini Dar es Salaam kujionea utendaji tangu lilipoboreshwa mwaka jana kwa kununuliwa na Serikali ndege mpya mbili.

Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga kuhakikisha anatekeleza suala hilo.


Pia, ametakaka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba za njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.

Vievile amesema ataagiza uchunguzi ufanywe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) utakaolenga kujua ukusanyaji mapato katika kipindi hicho.

Waziri Mkuu akasema Serikali haitakuwa tayari kushuhudia shirika hilo linakufa tena na kuwataka viongozi wahakikishe linaendeshwa kwa faida kwa manufaa ya Taifa.

MAJIBU YA MAALIM SEIF BAADA YA PROF LIPUMBA KUMTAKA WAYAMALIZE



Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Maalim Seif alitoa kauli hiyo kwenye ziara ya siku nne kwenye wilaya saba za mikoa mitatu ya Unguja.

Maalim alisema ataendelea kufuata taratibu za kisheria ili kuhakikisha chama kinamaliza moja kwa moja mgogoro aliodai umepandikizwa na CCM kupitia kwa Lipumba.

VURUGU ZATAWALA BUNGENI WABUNGE WAKIMPINGA RAIS..MABOMU YARINDIMA


Bunge la Afrika kusini jana lilijawa na vurugu kuipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.

Wakati akianza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa.

Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa,

Thursday, 9 February 2017

KATUNI KALI LEO..CHEKA,FURAHI,ONGEZA MAARIFA




WEMA, ZARI KUONANA 'LIVE' KWENYE AROBAINI YA MTOTO NILLAN

Akizungumza live kutoka Clouds Fm, Diamond ametamka rasmi kuwa staa Wema Sepetu ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo, kwa upande wa Zari Hassan nae amesema hana shida na ujio wa Wema Sepetu Kwenye Arobaini ya Nillan ambaye waliwahi kuingia kwenye bifu kipindi cha nyuma.

ANITHA ATENGEWA DAU LA ILIONI KUMI ACHEZE UTUPU HUKO NOLLYWOOD

anita-2  MSANII kutoka kiwanda cha filamu Nollywood, Anitha Joseph ametengewa dau la Naira milioni 1.4 (milioni 10 za Kibongo) ili acheze filamu za utupu nchini Marekani.
Kwa mujibu wa Jarida la Vanguard, Anitha anayependa kupiga picha akiwa ‘ameyabusti’ matiti yake, alikuwa akichati na jamaa kutoka Marekani, Kane na kumng’ang’aniza kucheza filamu hizo za utupu zitakazokuwa zikimuingizia

ZIGO LAMPAGAWISHA BOB JUNIOR KINOUMA NOMA

Stori: Na Andrew Carlos IJUMAA | ShowBiz
Ama kweli kuna watu wamejaaliwa! Msanii wa muziki Bongo, Bob Junior hivi karibuni alijikuta akishindwa kurekodi video ya wimbo wake wa Chukuchuku baada ya kuchanganywa na dada mmoja aliyemtumia

TUNDU LISSU NAYE ATOKA POLISI KWA DHAMANA YA SHILINGI MILIONI 20

https://www.youtube.com/watch?v=GdoKspsDky0
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.
Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu

ASKOFU GWAJIMA AMFYATUKIA MAKONDA SAKATA LA KUTAJWA DAWA ZA KULEVYA

https://www.youtube.com/watch?v=GdoKspsDky0Gwajima:- Namuomba Rais ambadilishie Kazi Makonda, hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu usiowapenda imemshinda. Sisemi amfukuze hapana nasema ambadilishie Kazi.

Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi

Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.

Gwajima : nilichelewa kidogo nikaamua kupanda helkopta yangu mpaka uwanjani kabisa.

LECEISTER CITY YAZIDI KULINDA HESHIMA YAKE



Leiceister city na Derby County wakichuana

Klabu ya soka ya Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima katika uwanja wake wa nyumbani wa king power kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Derdy County katika michuano ya mwaka huu ya FA CUP ukiwa ni mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya michuano hiyo.

Hadi dakika 90 za mchezo zina maliziaka timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-

JINSI MANJI ALIVYO WASILI KITUO CHA POLISI KATI CHA DAR ES SALAAM



Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.

Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.

Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi

advertise here