Saturday, 5 November 2016

POLIS WA KIKE WA KIISLAMU KUVAA IJABU SASA

Serikali ya Scotland imeidhinisha vazi la hijabu na kulijumuisha kwenye sare za maafisa wa polisi wa kike wa Kiislamu ili kuongeza idadi yao katika idara hiyo.

Mkuu wa idara ya polisi nchini humo Phil Gormley, ametoa maelezo na kubainisha furaha kubwa kwa kutangaza uamuzi huo, na kufahamisha nia yao kutaka kusaidiana na maafisa wa Kiislamu katika suala la usalama wa taifa.

Wednesday, 2 November 2016

AINA TATU YA MAWAZO YANAYOZUIA USHINDWE KUFANIKIWAA

Kiasili binadamu tumepewa uwezo mkubwa wa kufikiri ukitofautisha na wanyama wengine. Uwezo huu tulionao huwa unakuja hasa kutokana na matumizi ya mawazo au kufikiri kwetu. Kufikiri huko ambapo tunafanya kila siku na kila wakati ndipo kunapotufanya tuwe na maisha ya aina fulani, haijalishi yawe ya mafanikio au kushindwa.

Lakini hata hivyo wengi wetu huwa tunafikiri au tuna mawazo ya kimazoea na kushindwa kutambua kwamba hayo mawazo yetu pia yamegawanyika. Kwa mawazo yoyote uliyonayo mara huwa yamegawanyika katika sehemu. Kwa mfano unapowaza wazo fulani, wazo hilo linakuwa lipo moja

KAZI: MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA KABLA YA KUACHA KAZI

Leo hii karibu kila mtu aliyeajiriwa ukimuuliza je, unafurahia maisha ya kuajiriwa? Atakwambia hapana ila natamani kujiajiri, na endapo utaendelea kumuuliza ni kwa nini unatamani kujiajiri? Utamsikia anasema nataka kuwa huru na muda na pia nahitaji uhuru wa kipesa.

Majibu hayo kwa mtazamo wa wengi ni sawa, ila kuna kitu ambacho ni vyema ukakijua kabla ya kuamua kuacha kazi na kwenda kujiajiri.

Kujiajiri kuna hitaji ujasiri wa hali ya juu sana maana kuna changamoto zaidi ya kuajiriwa. Hivyo nakusihi  ufikirie kwa umakini sana suala zima la kuacha kazi kabla kwenda kujiajiri.

Na endapo utaamua kuacha kazi ya kuajiriwa bila ya kufikiria ipo siku utakuja kujutia uamuzi wako. Hivyo ni vyema ukafikiria mara mbili kabla ya kufanya maamuzi magumu.

Mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kuacha kazi.

1. Kuwa na nidhamu ya muda.
Kwa kuwa kwa sasa bado umeajiriwa, hivyo huna jukumu la kufanya maamuzi ya matumizi ya muda, Bali unafanya kazi kutokana na muda ambao muajiri wako ameamua yeye kukupangia kuweza kufanya kazi.

Na kwa kuwa umezoea kufanya kazi kutokana na amri ya mwajiri wako, hata pale ambapo utaamua kuacha kazi fahamu fika ya kwamba suala la kuwa na nidhamu ya muda kwako ni suala gumu, hivyo unatakiwa kufanya jitihada zako binafsi kadri iwezekanavyo hasa katika matumizi sahihi ya kufanya kazi hasa suala zima la uzalishaji wa mali au huduma.

Nazungumza suala zima la matumizi ya muda kwani hapa ndipo ambapo tunapata makundi mawili ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa. Hivyo ni jambo jema kuhakikisha unazingatia matumizi sahihi ya muda ili pindi utakapoacha kazi wewe ndiye ambaye utakuwa na jukumu la kupanga muda wa kufanya kazi na ni muda gani utakuwa ni wa kupumzika. Pia ikiwezekana ongeza matumizi sahihi ya muda mara mbili zaidi ya ulivyokuwa umeajiriwa.

2. Kutokuahirisha kufanya mambo ya msingi.
Utakuwa shahidi ya kwamba wakati umeajiriwa suala zima la uahirishaji wa kufanya mambo ya msingi lilikuwa ni suala gumu sana labda awe ameamua mwajiri wako. Kama ndivyo hivyo basi pale ambapo utakuwa umeamua mwenyewe kuacha kazi na kuamua kufanya kazi mwenyewe hivyo huna budi kuhakikisha ya kwamba suala zima la uhairishaji mambo linakuwa ni suala ambalo halina nafasi katika maisha yako.

Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi kwa kuamua kutenda bila kuahiirisha vitu vya msingi ama hakika utafika kilele cha mafanikio yako ndani ya muda mfupi. Ni vyema kulizingatia hili, kwani hili ndilo ambalo limewafanya watu wengi ambao waliacha kazi kuwa na maisha duni zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni waahirishaji wazuri wa vitu vya msingi

GABO KULIZIBA PENGO LA KANUMBA

Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba.

Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana.

Tuesday, 1 November 2016

MR BLUE HAITAJI MENEJA KATIKA MZIKI WAKE NINI MAONI YAKO

Msanii wa muziki wa kurap, Mr Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa kumsaidia katika kazi zake za muziki kwa kuwa tayari alishawahi kuwa na mameneja zaidi ya watatu ambao hawakumpatia mafanikio.
f1cbmr-Blue-ft-alikiba-mboga-saba

UJUMBE WA WEMA SEPETU KWA MISS TANZANIA MPYA

Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amedai mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016, Diana Edward alistahili kuchukua taji hilo.

Kupitia Instagram, Wema ameandika:

When You Nailed that question Properly, I knew that The Crown was Yours…. Congratulations mdogo wangu… You deserve it… And I have a very good feeling about Your performance in the

Monday, 31 October 2016

KIFO CHA MWANAMASUMBWI THOMASI MASHALI KUTOLEWA TAARIFA SIKU YA JUMA TANO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na upelelezi kwa kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.

Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema taarifa zilizopo kwa kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu, hivyo Jumatano nitatoa taarifa hiyo.

KIJUE ALICHOKITAMKA MAGUFULI HUKO KENYA

Rais Magufuli ambaye yuko nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo kabla ya Mkutano na waandishi wa habari leo October 31 2016 amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa

VIDEO:KEJERI YA NAY WA MITEGO KUHUSU MILLION 500 ZA IDRISS NA WEMA SEPETU

Nay wa Mitego ni kati ya Mastaa wa Tanzania ambao karibia kila wanachokifanya kwenye maisha yao hugeuka kuwa Headlines kubwa kutokana na style ya vitu wanavyofanya. Leo October 27, 2016 kupitia Instagram Rapa Nay wa Mitego a.k.a True Boy amepost video

KIPYA KUHUSU MISS TANZANIA 2016

Baada tu ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2016, Mrembo Diana Lukumay alianza kupokea msg za taarifa zilizosambazwa mitandaoni kuonyesha kwamba alifeli kidato cha nne lakini pia pamoja na hayo bado CV yake ilionyesha anayo degree.
Diana ameamua kuweka kila kitu wazi kwa kusema ‘Jina langu ni Diana Loi Lukumay, mmasai na

VIDEO : LICHA YA KUWA NA MVUA KUBWA HIVI NDIVYO DIAMONDPLATNUMZ ALIVYOVUNJA RECORD HUKO MALAWI

Ni habari iliyo njema kwa muziki wa Tanzania pale unapoona mwimbaji wake anaalikwa kwenda kutumbuiza kwenye taifa ambalo sio taifa linalotumia lugha ya Kiswahili lakini muziki wa bongofleva umeweza kupenya.
Mwimbaji Diamond Platnumz wa Tanzania alialikwa kwenda kutumbuiza Malawi Jumamosi ya

BREAKING NEWS:BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU TANZANIA IMETANGAZA RASMI KWA WANAFUNZI WOTE WALIOOMBA MKOPO KUANGALIA SASA MIKOPO WALIYOPANGIWA 2016/2017



Image result for OLAS.GO.TZ


Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Inawatangazia waombaji wote wa mwaka wa masomo 2016/2017 ,kuangalia mikopo waliyopangiwa.

Kama utahitaji kuangaliziwa jina lako kwa "usahihi" na "kasi ya ajabu" (ambapo utajibiwa ndani ya dk 1 tu) kama limepata mkopo tafadhali fanya yafuatayo;

Sunday, 30 October 2016

HESLB YAFAFANUA VIGEZO UTOAJI MIKOPO, WALIOKOSA SABABU ZATAJWA, WAPEWA NAFASI YA KUKATA RUFAA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017.

Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi

Wednesday, 26 October 2016

VIDEO DIAMOND PLATNUMZ AKITUONYESHA NYUMBA ALIYONUNUA HUKO SOUTH AFRIKA

Siku kadhaa zimepita toka msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz atangaze kuwa kanunua nyumba ya kuishi Afrika Kusini, huku baadhi ya watu wakidaiwa kutoa

Monday, 24 October 2016

UNAJUAJE KAMA UMEISHIWA MAJI MWILINI

UTAJUAJE KAMA UNA UPUNGUFU WA MAJI MWILINI?
Umeshawahi kwenda hospitali kumlalamikia daktari kuwa mwili wako hauna nguvu na unajisikia kuchokachoka sana na baada ya kukuchunguza, akakwambia huna tatizo lolote isipokuwa una upungufu wa maji mwilini tu?

Sunday, 23 October 2016

SABABU ZA KUHARIBIKA MIMBA

KATIKA makala ya afya wiki hii tuangalie sababu zinazosababisha mimba kuharibika.
Kuharibika kwa mimba ni  hali ya mwanamke kupata ujauzito na ukatoka kabla ya muda wake ambapo tatizo hili huangaliwa kabla ya kutimiza wiki 20 tangu kutungwa kwake.
Hali hiyo inapotokea huitwa kuwa mimba imetoka au imeharibika (Miscarriage).
Hali hii ya mimba kuharibika inakuwa tofauti kabisa na utoaji mimba ambapo kitendo cha kutoa mimba kinafanywa na binadamu kwa makusudi na huwa amedhamiria kufanya hivyo.

KUTANA NA MWANAMKE MNENE KULIKO WOTE DUNIANI

Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria

ANAYEDAIWA KUTOKA KIMAPENZI NA WEMA KWA SASA ADAI HAJUI IDRIS SULTAN

Model anayedaiwa kutoka kimapenzi na malkia wa filamu Wema Sepetu, Calisah amefunguka na kuzungumzia tetesi hizo ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii.
Kijana huyo ambaye tayari ameshaonekana mara kadhaa katika baadhi ya video za mastaa wa muziki nchini, amemmwagia sifa malkia huyo wa filamu huku akishindwa kuweka wazi kama ni kweli anatoka naye kimapenzi au la!.

“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe,” Calisah alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lakizima ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi mzuri,”
Pia kijana huyo alidai kuwa hamtambui Idris Sultan na hakumbuki kama Tanzania imewahi

DIAMOND, HARMONIZE, AY, DJ D-OMMY WASHINDA TUZO YA AEAUSA


Diamond Platnumz, Harmonize, AY na DJ D-Ommy wa Clouds FM wameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA zilizotolewa usiku wa kuamkia Jumapili huko New Jersey, Marekani.
Diamond ameshinda kipengele cha Best Male Single na pia kuungana na AY kwenye Best Collabo (Zigo Remix).

Harmonize ameshinda tuzo ya Best New Artist huku D-Ommy akishinda tuzo ya Dj bora.
Katika kushukuru kwa tuzo hiyo, Harmonize ameandika kwenye Instagram:

MAREHEMU MICHAEL JACKSON AMEINGIZA $825M MWAKA HUU

Forbes wametoa orodha ya mastaa waliofariki wanaoendelea kuingiza mkwanja mrefu zaidi. Mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson ndiye anayeongoza orodha hiyo akiwa ameingiza kiasi cha dola milioni 825
 Sababu ya kuongoza orodha hiyo imetajwa ni kufuatia uamuzi wa kuuzwa nusu ya hisa zake kampuni Sony/ATV inayomiliki nyimbo za The Beatles na kuingizia kiasi cha dola milioni 750.

advertise here