Monday, 31 October 2016

VIDEO:KEJERI YA NAY WA MITEGO KUHUSU MILLION 500 ZA IDRISS NA WEMA SEPETU

Nay wa Mitego ni kati ya Mastaa wa Tanzania ambao karibia kila wanachokifanya kwenye maisha yao hugeuka kuwa Headlines kubwa kutokana na style ya vitu wanavyofanya. Leo October 27, 2016 kupitia Instagram Rapa Nay wa Mitego a.k.a True Boy amepost video
mbili akiwazungumzia Wema Sepetu na Idris Sultan.
Kwa mujibu wa Video hizo Nay anasikika akihoji kilichomaliza pesa za mshindi huyo wa shindano la Big Brother Afrika msimu wa 2014 na kuondoka na mkwanja mrefu sana kiasi cha shilingi Milioni 500.
Baada ya ushindi wake Idris aliingia kwenye headlines za kudate na mastaa wengine akiwemo mshiriki mwenzake wa shindano la BBA Samantha ambaye waliachana na akaanza kudate na Wema Sepetu ambaye naye ziko stori kwamba wawili hao hawako pamoja japo hakuna aliyethibitisha wala kukanusha mpaka sasa.
Sasa Nay wa Mitego anauliza je zile Milioni 500 za Idris ni mwanamke gani amezimaliza kati ya Wema Sepetu au Samantha

No comments:

Post a Comment

advertise here