Monday 31 October 2016

VIDEO : LICHA YA KUWA NA MVUA KUBWA HIVI NDIVYO DIAMONDPLATNUMZ ALIVYOVUNJA RECORD HUKO MALAWI

Ni habari iliyo njema kwa muziki wa Tanzania pale unapoona mwimbaji wake anaalikwa kwenda kutumbuiza kwenye taifa ambalo sio taifa linalotumia lugha ya Kiswahili lakini muziki wa bongofleva umeweza kupenya.
Mwimbaji Diamond Platnumz wa Tanzania alialikwa kwenda kutumbuiza Malawi Jumamosi ya
weekend iliyopita na hata yeye mwenyewe amefurahishwa na mwitikio wa Malawi kwenye muziki wake.
screen-shot-2016-10-30-at-11-56-27-pm
Nilipokua nikiimba ‘nasema nawe’ leo nimegundua kuwa wasichana wa kimalawi ni hatari sana kwenye kukatika …..we unahisi Wasichana wa nchi ipi wanashika number moja kwenye kukatika? – caption ya Diamond kwenye hii picha
Diamond ameandika ‘Licha ya Mvua kunyesha na kuharibu stage na system yote muziki lakini mliamua kuvumilia na kunisubiria kuanzia usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi nilipopanda na kuanza show yangu…
Imefanya niwapende na kuwathamini kuliko mliyofikiria MALAWI…shukran sana kwa mapenzi yenu kwangu, natumai Show mliifurahia…tukutane tena wakati mwingine……NIGERIA see you this weeknd‘ – Diamond
screen-shot-2016-10-30-at-11-56-39-pm
screen-shot-2016-10-30-at-10-22-57-pm
.
screen-shot-2016-10-30-at-10-23-39-pm
LOGO MOTION WASAFI RECORD

No comments:

Post a Comment

advertise here