Rais
Magufuli ambaye yuko nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili
ambapo kabla ya Mkutano na waandishi wa habari leo October 31 2016
amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi
lililoandaliwa kwa
heshima yake na baadaye kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
heshima yake na baadaye kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Rais
Magufuli akizungumza na waandishi wa habari Ikulu ya Nairobi nchini
Kenya amesema Kenya ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania
ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika ambapo amebainisha
kuwa takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa Kenya
ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania
ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.
Aidha Rais
Magufuli amebainisha kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya
imeongezeka kutoka Shilingi za Kitanzania Bilioni 652.9 hadi Shilingi za
Kitanzania Trilioni 2.044.
>>>’Naomba
niwahakikishie kuwa uhusiano na ushirikiano wetu ni mzuri na utaendelea
kuwa mzuri zaidi, na kwetu sisi Tanzania, Kenya ndio nchi ya kwanza kwa
uwekezaji kuliko nchi zote za Afrika’;-Rais Magufuli.
>>>’Tunashirikiana
vizuri katika uchumi, watu wetu wanafanya kazi pamoja, yapo makabila
yetu ambayo yanaingiliana kwa shughuli zao za kila siku na hata
wanyamapori wetu wanazunguka katika nchi zote mbili bila kujali
mipaka’;- Rais Magufuli.
Kwa upande
wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli
kwa kukubali mwaliko wake na amemhakikishia kuwa Kenya itaendeleza na
kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Tanzania.
>>>’Kwetu
sisi Tanzania ni ndugu zetu, ni kaka na dada zetu tunao ushirikiano wa
siku nyingi na wa kidugu na tutahakikisha tunauendeleza ushirikiano na
uhusiano huu mzuri ulioasisiwa na wazee wetu’;–Rais Kenyatta.
Rais
Kenyatta amesema Tanzania na Kenya ni nchi zinazofanana kwa mambo mengi
muhimu ikiwemo kubadilishana uongozi wa Serikali kwa njia ya amani na
ameongeza kuwa katika mazungumzo yao wamekubaliana kuwa nchi hizi
zitaendelea kuzisaidia nchi nyingine za Afrika Mashariki zinazokabiliwa
na matatizo mbalimbali.
Aidha,
Rais Kenyatta amesema Kenya itaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kutekeleza miradi ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile
barabara ya Bagamoyo (Tanzania) hadi Malindi (Kenya) pamoja na mambo
mengine ambayo Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili
(Joint Commission Cooperation) itayaainisha
ULIKOSA KUONA VIDEO MAGUFULI AKIZUNGUMZIA SUKARI VIDEO HII HAPA
No comments:
Post a Comment