Model
anayedaiwa kutoka kimapenzi na malkia wa filamu Wema Sepetu, Calisah
amefunguka na kuzungumzia tetesi hizo ambazo zimekuwa zikisambaa katika
mitandao ya kijamii.
Kijana huyo ambaye tayari ameshaonekana mara kadhaa katika baadhi ya
video za mastaa wa muziki nchini, amemmwagia sifa malkia huyo wa filamu
huku akishindwa kuweka wazi kama ni kweli anatoka naye kimapenzi au la!.
“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni
mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo
Wema mwenyewe,” Calisah alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Siwezi
kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lakizima ujue kuwa
Wema ni mzuri na mimi mzuri,”
Pia kijana huyo alidai kuwa hamtambui Idris Sultan na hakumbuki kama
Tanzania imewahi
kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika.
kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika.
“Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?,” aliuliza kijana huyo.
Malkia huyo wa filamu toka aachane na mshindi huyo wa Big Brother Afrika 2014, hajaweka wazi mahusiano yake mapya.
No comments:
Post a Comment