Sunday, 23 October 2016

DIAMOND, HARMONIZE, AY, DJ D-OMMY WASHINDA TUZO YA AEAUSA


Diamond Platnumz, Harmonize, AY na DJ D-Ommy wa Clouds FM wameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA zilizotolewa usiku wa kuamkia Jumapili huko New Jersey, Marekani.
Diamond ameshinda kipengele cha Best Male Single na pia kuungana na AY kwenye Best Collabo (Zigo Remix).

Harmonize ameshinda tuzo ya Best New Artist huku D-Ommy akishinda tuzo ya Dj bora.
Katika kushukuru kwa tuzo hiyo, Harmonize ameandika kwenye Instagram:
Najivunia kuwa mtanzania navyenye wenye Tanzania yao wanavyo ni support katika nyanja tofauti sina chakuwalipa ila nitahakikisha nafanya kile mnacho kipenda Asante kwa kunipigia kura na kuifanikisha tuzo hii nyingine africa kutuwa Tanzania……🙏🙏🙏 pia team mzima #Wcb kwa kuhamasisha upigaji kura M/mungu awabariki sanaa……..!!! uongozi mzzimaa #WCB kwakuwa nami bega kwa bega kuniongeza Mama Chiiiiibu @kendrah_michael umekuwa ukishauri mambo mengi sanaaaa mama angu sina cha kukulipa and mama Harmo umekuwa ukiniombea sana……!!!! niishie hapo kwaleo ila amini kuwa nina furaha naamini kuwa hii ni hatua moja wapo…….🙏 #Raj ♡
Tuzo hizo zilizokuwa zikirushwa live kupitia Trace Urban, zimetolewa saa chache baada ya zile za MTV MAMA ambapo hakuna msanii wa Tanzania alishinda.

No comments:

Post a Comment

advertise here